BWENI LA WAVULANA LATEKETEA KWA MOTO KIGAMBONI

0
980

|   Na Mwandishi wetu              |          


Bweni la wavulana katika Shule ya Sekondari Kisarawe 11 iliyopo Wilaya ya Kigamboni limeteketea kwa moto usiku wa kuamkia jana.

Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Sara Msafiri, amesema leo kuwa tukio hilo lilitokea saa 4:30 usiku juzi na hakuna kifo wala majeruhi.

Amesema katika bweni hilo walikuwa wanaishi wanafunzi 29 wa kidato cha pili na wakati tukio linatokea walikuwa darasani wakijisomea.

“Wanafunzi wako salama lakini vitu vyao vimeteketea vyote, tunachokifanya sasa ni kurejesha huduma za kibinadamu wakati tukijipanga kujega bweni jipya,” amesema Sara.

Amesema uchunguzi unaendelea kubaini chanzo cha moto huo na kwasasa wanafunzi hao wanalala darasani.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here