25.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

BUWASA yaagizwa kuzikatia maji Taasisi za Serikali Bukoba

Na Renatha Kipaka, Bukoba

Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Albert Chalamila amtoa maagizo kwa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira (BUWASA) kutoa notisi kwa Taasisi zote zinazodaiwa na endapo hazitalipa kwa wakati wasitishiwe huduma.

Chalamila ametoa agizo hilo jana wakati akizungumza na Mamlaka zinazotoa huduma ya maji kwa Wananchi zilizopo mtaa wa Majengo Kata Kashai Manispaaa ya Bukoba.

“Niseme tu Kama kuna taasisi yoyote ya serikali inadaiwa, ipeni notisi leo weka nukuu ya vifungu vyako juu ya uendeshaji na baada ya muda mkate maji, katika hili huwa sidanganyi,” amesema Chalamila.

Amesema baada ya kukatiwa maji hakuna taasisi itakayo sumbua kwa hatua hiyo na huduma kutoendelea kwenye maeneo yao.

“Hakuna mtu atakayesumbua na baada ya hapo mimi nitajua pa kuwasiliana na mamlaka zao ili madeni yalipwe,” amesema Chalamila.

Amesema makusanyo yanayopatikana kwenye mamlaka hiyo yanasaidia kujiendesha yenyewe kama watoa huduma kwa wananchi wanaotumia maji

Aidha, amesema ili kuendelea kustawi na kufanya huduma kuwa bora lazima ufuatiliaji wa miradi uwe wa uhakika na vifaa vinavyotumiwa.

Mkurugenzi wa Mamlaka hiyo, Mhandisi John Sirati amesema huduma ya maji inatolewa kwenye kata 14 zilizopo Manispaa ya Bukoba.

Ameongeza kuwa uzalishaji wa maji ni lita milioni 18 kwa siku kutoka kwenye chanzo kikuu cha Ziwa Victoria na mahitaji ni lita milioni 13

“Kwa siku tunazalisha lita milioni 18 ambazo zinatoka kwenye chanzo chetu kikuuu ambacho ni ziwa Victoria tuliweka eneo la Bunene kata Bakoba na mahitaji ni lita milioni 13,” amebainisha Sirati.

Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa huo, Projestus Rubanzibwa amesema,ni vyema taasisi za umma kuwasilisha taarifa za utekelezaji kila robo mwaka ili kufahamu kinachoendelea.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles