27.3 C
Dar es Salaam
Monday, December 4, 2023

Contact us: [email protected]

BUSHOKE AJIVUNIA ‘NGOMA YA UKAYE’

Na GLORY MLAY

MKALI wa Bongo Fleva, Ruta Maxmilian ‘Bushoke’, amesema matumaini yake makubwa yapo kwenye video yake mpya ya ‘Ngoma ya Ukaye’ ambayo anaamini itamtambulisha upya kwenye tasnia ya muziki.

Msanii huyo alisema kwamba, baada ya kuwaahidi mashabiki wake kuwa atarudi kwa kishindo, ndivyo alivyofanya katika ngoma yake mpya aliyoitambulisha hivi karibuni.

“Mashabiki zangu ndio nimerudi kama hivyo mlivyoona na kusikia, mimi ndiye yule yule Bushoke mliyemzoea kipindi cha nyuma, matumaini yangu yapo kwa mashabiki ambao ni wadau wangu wakubwa wa kazi ninazozifanya,” alisema.

Alisema anamshukuru Mungu kwa kumvusha katika changamoto mbalimbali alizokumbana nazo pale alipokua mbali na muziki, hata hivyo ameahidi kutopotea tena kwa muda mrefu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
580,000SubscribersSubscribe

Latest Articles