20.8 C
Dar es Salaam
Saturday, August 20, 2022

Burundi yawaita wakimbizi nyumbani

prefere-ndayishimiyePATRICIA KIMELEMETA-DAR ES SALAAM

SERIKALI ya Burundi imewataka wakimbizi wanaoishi katika nchi mbalimbali kurudi nchini mwao kwa sababu hali ya usalama ni nzuri.

Kauli hiyo ilitolewa   Dar es Salaam jana na Balozi wa Burundi  nchini, Pre’fere’ Ndayishimiye.

Alisema   vita  iliyojitokeza mwaka jana wakati wa Uchaguzi Mkuu imekwisha, kilichobaki ni wananchi kuungana na kuleta maendeleo kwenye nchi yao.

Alisema  taarifa zinazotolewa na baadhi ya watu za kuwapo   vurugu katika  nchi hiyo si za kweli na   zinapaswa kupuuzwa.

“Ninawaomba wananchi wote wa Burundi wanaoishi katika maeneo mbalimbali ndani na nje ya Tanzania wakiwamo ‘Wahutu’ na ‘Watutsi’ kurudi nchini kwetu sababu hakuna vita wala vurugu na kwamba hali ya usalama ni nzuri,”alisema Ndayishimiye.

Aliongeza kuwa hali ya Burundi ni shwari na kilichobaki ni propaganda zinazotolewa na watu wachache wenye malengo ya kuichafua nchi hiyo huku wakijua kuwa wanachokisema siyo cha kweli.

Alisema   serikali ya nchi hiyo inaendelea kufanya mazungumzo na vyama vya upinzani   kuondoa tofauti zilizojitokeza na kujipanga upya kwa ajili ya kuleta maendeleo kwa wananchi bila ya kujali tofauti za kisiasa.

Balozi Ndayishimiye alitumia mkutano huo kuwataka wawekezaji duniani kote kujitokeza kwa wingi chini humo kuwekeza kwenye nyanja mbalimbali za  uchumi na  jamii  kurahisisha maendeleo.

Akizungumza katika mkutano huo, Katibu Mkuu wa chama tawala cha NCDD-FDD, Evariste Ndayishimiye alisema chama hicho kimejipanga kupata ushindi kwenye uchaguzi mkuu ujao 2020.

Alisema hivi sasa Serikali kwa kushirikiana na chama tawala wameanza mazungumzo na vyama vya upinzani  kuhakikisha uchaguzi huo unakuwa wa amani na utulivu ili kuepusha umwagaji wa damu, vurugu na machafuko.

Alisema tofauti zilizojitokeza zimefanyiwa kazi na jopo lililoteuliwa kwa ajili ya usuluhishi wa mgogoro huo likiongozwa na Rais mstaafu wa Tanzania, Benjamini Mkapa.

Kutokana na hali hiyo, waangalizi wa amani wamekuwa wakifika Burundi mara kwa mara   kuangalia hali ya usalama, hivyo kuwatia moyo.

“Tunamshuruku Rais Mkapa kwa kushirikiana na viongozi wengine ambao waliteuliwa kuongoza vikao vya usuluhishi nchini kwetu, hali iliyosaidia mpaka sasa kuwapo   amani na utulivu,”alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
199,058FollowersFollow
551,000SubscribersSubscribe

Latest Articles