24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Burundi yatoa hati ya kumkamata   Buyoya

BUJUMBULA, Burundi



SERIKALI ya hapa  imetoa hati ya  kimataifa ya kumkamata Rais wake wa zamani,  Pierre Buyoya na maofisa wengine 16, kuhusiana na mauaji ya Rais wa kwanza wa nchi hii, Melchior Ndadaye aliyechaguliwa kwa njia ya kidemokrasia.

Mwendesha Mashtaka Mkuu,  Sylvestre Nyandwi alisema juzi kwamba  uchunguzi umebaini kuwa watu hao walihusika katika kupanga na kutekeleza mauaji  ya  Ndadaye ambaye pia alikuwa  kiongozi wa kwanza  kutoka jamii ya Wahutu.

Mauaji hayo yalifuatiwa na machafuko makubwa ya ukabila ambako   zaidi ya watu 300,000 waliuawa.

Buyoya kwa wakati huu ni mwakilishi wa Umoja wa Afrika nchini Mal na ni mtu anayeheshimiwa   Afrika na katika jumuiya ya kimataifa.

Buyoya, Mtutsi aliyeingia madarakani kupitia mapinduzi ya  jeshi mwaka 1987, alikubali kushindwa na Rais Ndadaye katika uchaguzi wa mwaka 1993.

Hata hivyo Rais  Ndadaye alikaa madarakani kwa miezi minne tu kabla ya  akuuawa na kundi la wanajeshi Watutsi wenye misimamo mikali katika jaribio la mapinduzi lililoitumbukiza nchi  katika mzozo ambao athari zake zinaendelea hadi leo.

Katika hati hiyo, serikali inazitaka nchi wanakoishi watuhumiwa hao kuwakamata na kuwarejesha nchini hapa  ikisema ni muhimu watu hao kuhojiwa kuhusu mchango wao katika mauaji ya Rais Ndadaye.

Miongoni mwa watuhumiwa 16 pamoja na   Buyoya, 11 walikuwa maofisa wa jeshi  na watano waliobakia walikuwa raia wenye uhusiano ya karibu na rais huyo wa zamani.

Serikali ya sasa    inaongozwa na Chama Cha Cndd-FDD cha Rais Pierre Nkurunziza, ambacho ni tawi la kundi la zamani la waasi Wahutu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles