22.9 C
Dar es Salaam
Sunday, June 23, 2024

Contact us: [email protected]

Burundi yailalamikia Rwanda

Pg 2NA TUNU NASSOR, DAR ES SALAM

SERIKALI ya Burundi, imeendelea kuilaumu  Rwanda kwa like inachodai inachochea machafuko nchini mwao, hali ambayo inahatarisha usalama wa wananchi wao.

Akizungumza na waandishi wa habari  jijini Dar es Salaam juzi, Msemaji wa Serikali ya Burundi, Gervais Abayeho alisema wana ushahidi wa kutosha  Rwanda inatoa mafunzo na kuwapa silaha vijana ili kwani nia ya kufanya mipango ya kupindua utawala  nchi hiyo.

“Kuna vijana wamejisalimisha kwa Serikali ya Burundi na kushuhudia Rwanda ndiyo mfadhili wao mkuu kwa kuwapa mafunzo na silaha ,”alisema Abayeho.

Alisema hata vyombo vya Umoja wa Mataifa (UN) na Umoja wa Afrika (AU), vilifika Burundi kufanya uchunguzi na kujiridhisha madai hayo yana ukweli.

Alisema askari wa nchi yake, waliwahi kukamata gari linalomilikiwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia  Wakimbizi (UNHCR), likiwa limetengenezwa kwa ajili ya kuficha silaha.

Baada ya kulikamata gari hilo likiwa na silaha, dereva aliyekuwa analiendesha alikiri kuingiza silaha kwa mara ya tatu nchini Burundi kabla ya kukamatwa.

Kuhusu hali ya usalama, alisema imetulia na kuwataka wananchi waliokimbia kurudi kujenga nchi yao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles