21.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, August 16, 2022

BURUNDI: WANAFUNZI WALIOKAMATWA WAACHIWA HURU

Burundi imewaachilia huru wanafunzi watatu wa kike ambao walikamatwa wakishutumiwa kuichafua kwa kuichorachora picha ya rais wa nchi hiyo Pierre Nkurunziza kwenye vitabu vyao vya shule.

Kushikiliwa kwa wasichana hao takribani majuma mawili yaliyopita kwa shutuma za kumtusi rais kulizusha kampeni mitandaoni za kutaka wasichana hao waachiliwe, kampeni iliyokua na jina #FreeOurGirls, watu wakituma picha kwenye mitandao ya Twitter.

Kwa mujibu wa Waziri wa Sheria Aimée Laurentine Kanyana, amesema wasichana hao wenye miaka 15,16 na 17 wameachiwa huru kwa muda.

”Tunataka wazazi waboreshe elimu ya watoto wao .Tunawakubusha watoto kuwa wanapaswa kuheshimu mamlaka,na kuwa umri wa kuwajibishwa ni miaka 15,” alisisitiza Waziri Kanyana

Wasichana hao walikamatwa wakiwa katika shule ya ECOFO iliyopo katika mkoa wa kaskazini mwa Burundi tarehe 12 mwezi Machi ,2019

Awali walishitakiwa wakiwa wanafunzi saba, lakini wanne wakaachiliwa huru.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,814FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles