31.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 11, 2024

Contact us: [email protected]

Bunge lashauri kufungwa CCTV kamera reli ya SGR

Na Nora Damian, Mtanzania Digital

Kamati za Kudumu za Bunge za miundombinu na Bajeti zimelishauri Shirika la Reli nchini (TRC) kufunga kamera za usalama (CCTV) na kujenga uzio katika njia ya reli ya SGR ili kudhibiti wahalifu wanaohujumu miundombinu yake.

Ushauri huo umetolewa leo Novemba 10,2024 na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Selemani Kakoso, baada ya kukagua miundombinu ya reli hiyo kutoka Dodoma hadi Dar es Salaam.

Amesema Serikali imewekeza fedha nyingi katika mradi huo na kuwataka Watanzania kulinda miundombinu ya reli hiyo ili shirika liendelee kustawi.

“Watu wameanza kukata nyaya za umeme wanahujumu reli ambayo uwekezaji wake ni mkubwa, tunashauri shirika lijenge mifumo ya ‘fensi’ na kamerabza CCTV ziwekwe njia yote.

“Mradi huu ni Watanzania kila mtu alinde miundombinu iliyowekezwa ili shirika liendelee kustawi iletwe tija ambayo italinufaisha taifa,” amesema Kakoso.

Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, Oran Njeza, amesema wameridhika na mwenendo wa ujenzi wa reli hiyo na kulitaka shirika hilo liharakishe kukamilisha vipande vilivyobaki pamoja na kuiboresha reli ya zamani ya MGR.

Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi, Ludovick Nduhiye, amesema watafanyia kazi maelekezo yaliyotolewa na kamati hizo ili kuongeza ufanisi katika shirika hilo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles