24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Bunge la EALA kuanza leo Z’bar

ealaNa Muhammed Khamis (UoI) -Zanzibar

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein anatarajiwa kufungua mkutano wa kikako cha tano cha Bunge la Afrika Mashariki (EALA) utakaoanza leo visiwani hapa.

Akizungumza na waandishi wa habari jana mjini Unguja, Spika wa Bunge la Afrika Mashariki, Daniel Kidega alisema kikao hicho kitajadili na kupitisha miswaada mitatu.

Alisema miswaada hiyo ni ile ya usawa wa kijinsia na maendeleo kwa nchi za EAC, uzuiaji wa usafirishaji haramu wa binadamu vitendo ambavyo vimekithiri katika miaka ya hivi karibuni.

“Kama tunavyojua suala la biashara haramu ya binaadamu ipo katika nchi mbali mbali na wananchi wengi wanatoka katika nchi za Afrika Mashariki na kwenda nchi za Ulaya kwa hivyo hili nayo linahitaji kujadiliwa kwa kina” alisema Spika Kidega

Alisema suala hilo linahitaji mjadala mpana kutokana na uzito wake na hivyo wabunge wa bunge hilo watajadili na kuona namna gani ya kukabiliana na changamoto iliyopo juu ya biashara hiyo ambayo inapaswa kushughuulikiwa na kuwekewa mikakati madhubuti.

Kwa upande wake Mbunge wa Bunge hilo kutoka Tanzania, Makongoro Nyerere, alisema ni utaratibu wa kawaida wa EALA kufanya vikao vyake katika nchi za Afrika Mashariki ambapo Zanzibar ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles