31.2 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Bunge kujadili zaidi miswada ya sheria

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu.

Na WAANDISHI WETU, DODOMA

KIKAO cha nne cha Bunge la 11 kinatarajia kuendelea leo mjini hapa baada ya mapumziko ya siku tatu yaliyoanza Ijumaa wiki iliyopita.

Leo baada ya kipindi cha maswali na majibu, wabunge wataendelea na mjadala wa Muswada wa Sheria ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali wa Mwaka 2016 na Muswada wa Sheria ya Usimamizi wa Wanataaluma wa Kemia wa mwaka 2016.

Miswada hiyo miwili iliwasilishwa mwishoni mwa wiki na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu.

Baada ya miswada hiyo kujadiliwa na kuhitimishwa leo, kesho wabunge wataanza na kipindi cha maswali na majibu na baadaye itawasilishwa miswada miwili ambayo ni Muswada wa Sheria ya Taasisi ya Utafiti wa Kilimo wa Mwaka 2016 na Muswada wa Sheria ya Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi wa Mwaka 2016.

Miswada hiyo itajadiliwa kesho na keshokutwa kabla ya Bunge kuahirishwa Ijumaa wiki hii.

Bunge   lilianza Septemba 6 mwaka huu kwa kipindi cha maswali na majibu kabla ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye, kuwasilisha Muswada wa Sheria ya Upatikanaji wa Taarifa wa Mwaka 2016.

Muswada huo ulipitishwa na Bunge baada ya kujadiliwa na wabunge kwa siku mbili ingawa wabunge wa upinzani waliupinga kwa kile walichosema unalenga kuvikandamiza vyombo vya habari kutokana na adhabu zilizomo kuhusu wanaopotosha taarifa.

Baada ya Bunge kupitisha muswada huo, Septemba 8 mwaka huu, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi, aliwasilisha Muswada wa Sheria ya Uthamini na Usajili wa Wathamini wa Mwaka 2016 ambao nao ulipitishwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles