27.3 C
Dar es Salaam
Monday, December 4, 2023

Contact us: [email protected]

Bunge  EALA kujadili muswada vifaa vya plastiki

eala-rwanda-chapter-chairperson-patricia-hajabakigaMuhamed Khamis (UoI) -Zanzibar

BUNGE la Afrika Mashariki (EALA) linaloendalea na vikao  visiwani hapa, limepokea  muswada wa kuzuia matumizi ya vifaa vinavyotokana na plastiki   na kusomwa kwa mara ya kwanza.

Akiwasilisha kwa mara ya kwanza muswada huo, mbunge   kutoka Rwanda, Parricia Hajabakiga alisema utekelezaji wa sheria hiyo utasaidia kwa kiasi kikubwa kudhibiti bidhaa za plastiki ambazo huharibu mazingira.

Alisema lengo la kubana na kuzuia matumizi yote ya vifaa vya  plastiki zikiwamo taka za viwandani, hospitali, maeneo ya ujenzi na maeneo mbalimbali yanayoambatana na matumizi hayo.

Mbunge huyo alisema licha ya ongezeko la athari mbaya za mazingira zinazohatarisha afya za watumiaji wa bidhaa hizo,  bado hali hiyo inaendelea kuongezeka siku hadi siku kutokana na bidhaa hizo.

Alisema bidhaa za plastiki athari zake ni kubwa katika mazingira na  baadhi ya nchi zimeweza kudhibiti na hivyo kusaidia usafi na kudhibiti uharibifu wa mazingira.

Hajabakiga  alisema muswada huo utaweka misingi imara ya kudhibiti mazingira kubaki salama kwa kuzuia kuzalisha bidhaa za plastiki ambazo zinaathiri vibaya mazingira hasa kwa kuzingatia bidhaa hizo huchafua hali ya hewa kutokana na moshi wake ingawa  bidhaa zenyewe kwa mfano mifuko, huwa haziozi na hivyo kufanya ardhi iwe kavu.

“Lengo jengine la muswada huu ni kuwaleta karibu wanamazingira rafiki  waweze kusimamia na kujua matumizi mbadala ya vifaa vilivyozalishwa kwa plastiki,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
580,000SubscribersSubscribe

Latest Articles