26.2 C
Dar es Salaam
Monday, October 3, 2022

BUNDUKI YA KIVITA YAOKOTWA VICHAKANI

Eliya Mbonea, Arusha

Bunduki ya kivita aina ya AK 47, ikiwa na risasi nne ndani imeokotwa ndani ya vichaka katika Kijiji cha Naan, Wilaya ya Ngorongoro mjini Arusha.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Mei 29, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Ramadhani Ng’anzi amethibitisha kuokotwa kwa silaha hiyo na kuongeza kuwa Jeshi la Polisi linaendelea kumsaka mmiliki wake.

“Mbali na bunduki hiyo, pia tumekamata pikipiki saba zinazodhaniwa kuwa ni mali ya wizi na watuhumiwa saba kupitia msako tuliofanya hivi karibuni,” amesema.

Kamanda Ng’anzi amezitaja mali zilizokamatwa kuwa ni televisheni sita, camera tatu, lensi mbili za camera, fedha taslimu Sh 915,000 na vitu vingine vya ndani na vifaa ofisini.

Pamoja na mambo mengine, Kamanda Ng’anzi amewaomba wakazi wa Arusha waliowahi kuibiwa kufika kituoni hapo ili kukagua kama wanaweza kutambua mali zao.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,573FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles