BUNDA SACCOS HATARINI KUFILISIKA

0
1749

Na RAPHAEL OKELLO – BUNDA


MAKAMU  Mwenyekiti wa Chama cha Akiba na Mikopo cha Bunda Saccos, Abas  Kakwaya  amewataka  wanachama 122 wa chama hicho kurejesha haraka Sh milioni 300 wanazodaiwa   ili kukinusuru chama hicho kufilisika.

Alisema  miongoni mwa wadaiwa wakubwa ni waliowahi  kushika nadhifa ya uenyekiti na  watumishi wa Saccos hiyo akiwamo meneja.

Kwa mujibu wa Abas, Saccos hiyo ilikuwa na watumishi sita kufikia mwanzoni mwa mwaka huu lakini kutokana  na kukopa na kushindwa kulipa wametoroka na kubakia mtumishi mmoja tu kwa sasa. Alisema  taarifa zao zote zimekwisha kupelekwa  polisi.

Akizungumza  katika mkutano  wa dharura  wa Saccos hiyo juzi, alisema wenyeviti hao na watumishi wasiofika watu 10 wanadaiwa  takriban Sh milioni 100 kati ya wanachama 122 wenye madeni.

Hata hivyo, alisema  Saccos hiyo inadaiwa na wanachama wake  akiba ya Sh  milioni 230. Mkutano huo uliwataka wanachama hao wawe na subira wakati madeni yanaangaliwa jinsi ya kurejeshwa.

Abas alisema   wanaoidai Saccos hiyo watarejeshewa fedha zao kidogo kidogo kadri zitakavyokusanywa.

Makamu mwenyekiti huyo alisisitiza a kwamba Bunda Saccos haijafilisika ingawa imesimamisha huduma ya kutoa mikopo ingawa  huduma nyingine zinaendelea.

“Ieleweke kwamba tumesimamisha tu huduma ya kutoa mikopo, tutaendelea na huduma yetu ya uwakala wa M pesa na huduma nyingine.

“Mtumishi wetu na bodi ya Saccos anaendelea na kazi kama kawaida kwa hiyo wanachama Msihofu,” alisisitiza Abas.

Katika mkutano huo, Abas alisema bodi  inaingia mkataba wa kukusanya madeni hayo na Kampuni ya Makama Investiment.

Alisema lengo la kufanya hivyo ni kuinusuru Saccos hiyo kubwa wilayani Bunda kutowekwa  chini ya Mfilisi.

Aliwataka wenyeviti na watumishi hao kuwa mfano kwa wanachama wengine kurejesha mikopo yao kwa haraka.

Mmmoja wa wajumbe, Siri Makanaki alisema wenyeviti   na watumishi wa Saccos wamechangia kwa kiwango

kikubwa kuifikisha Saccos hiyo katika hali mbaya.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here