26.2 C
Dar es Salaam
Monday, October 3, 2022

BULEMBO: MPINA ANA MPANGO WA KUIONDOA CCM MADARAKANI

Maregesi Paul, Dodoma

Mbunge wa kuteuliwa, Abdallah Bulembo (CCM), amesema Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina ana mpango maalumu wa kuiondoa Chama Cha Mapinduzi (CCM), madarakani.

Akichangia bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2018/19, Bulembo amesema kama operesheni sangara inayofanyika katika Ziwa Victoria ikiendelea CCM itakuwa na wakati mgumu wa kuwaomba kura wananchi katika Uchaguzi Mkuu na Serikali zaMmitaa unaotarajia kufanyika mwakani.

“Kuna haja operesheni hiyo isimame ili kuwaokoa wavuvi ambao wanaathiriwa na operesheni hiyo,” amsema Bulembo.

Kwa upande wake Mbunge wa Viti Maalumu, Dk. Wale Semesi (Chadema), naye amelalamikia operesheni hiyo na kutaka iundwe tume kuichunguza kwa sababu inaathiri wavuvi kama ilivyofanyika wakati wa operesheni tokomeza.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,573FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles