31.7 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

BULAYA: MAKONDA KAMATA ‘MAPAPA’

Na MAREGESI PAUL – DODOMA

MBUNGE wa Bunda Mjini, Esther Bulaya (Chadema), amemtaka Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, kuanza kuwakamata wafanyabiashara wakubwa ‘mapapa’ wanaojihusisha na dawa za kulevya.

Alisema pamoja na kuunga mkono jitihada za Makonda, kinachotakiwa sasa ni kuwakamata wafanyabiashara hao wakubwa aliowaita mapapa kwa kuwa ndio chanzo cha uwapo wa dawa hizo nchini.

Bulaya aliyasema hayo bungeni jana, alipokuwa akichangia taarifa ya shughuli za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Masuala ya Ukimwi ya mwaka 2016/17, iliyowasilishwa na Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Dk. Jasmin Tisekwa.

“Mimi sipingani na upambanaji wa dawa za kulevya, nawashauri wahusika mumshauri Rais ateue kamishna wa kupambana na dawa za kulevya.

“Namshauri mdogo wangu Makonda, hao anaowakamata na kuwaweka ndani ni watu wadogo sana, badala yake awakamate mapapa ambao ndio wanaoingiza dawa hizo.

“Makonda akamuone Mama Leila kule gerezani, akamweleze dawa zinavyoingizwa nchini kwa sababu hao anaowakamata ni wale wanaotakiwa kuwa Mwananyamala au Muhimbili kwa ajili ya kupatiwa matibabu,” alisema Bulaya.

Pamoja na hayo, aliitaka Serikali ipeleke dawa katika vituo vya kutibu waathirika wa dawa za kulevya kwa kuwa taarifa zinaonesha havijapata dawa tangu Novemba, mwaka jana.

Wakati huo huo, Bulaya alisema wauzaji wa dawa za kulevya wameanza mkakati wa kuanza kuziuza katika vituo vya kutibu waathirika wa dawa hizo kwa kuwa mtaani wameanza kudhibitiwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles