25.6 C
Dar es Salaam
Sunday, January 5, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

BULAYA AUGUA GHAFLA MAHABUSU, AHAMISHIWA MUHIMBILI    

NA SHOMARI BINDA -MUSOMA

MBUNGE wa Bunda Mjini, Esther Bulaya (Chadema), amehamishiwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa ajili ya matibabu baada ya kuugua ghafla akiwa mahabusu kwenye Kituo cha polisi Tarime alipokuwa ameshikiliwa.

Baada ya kuhudumiwa kwenye Hospitali ya Wilaya ya Tarime hali yake ilibadillika ambapo inadaiwa alianza kupumua kwa shida na baadaye alihamishiwa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mara kabla ya kupewa rufaa ya kupelekwa Muhimbili.

Akizungumza na waandishi wa habari eneo la hospitali hiyo, Mbunge wa Viti maalumu Mkoa wa Mara, Joyce Sokombi (Chadema) alisema akiwa mahabusu kwenye kituo cha Tarime, Bulaya alishindwa kupumua vizuri na mwili kuishiwa nguvu ambapo alikimbizwa kwenye hospitali ya wilaya na kupata matibabu lakini hali yake bado haikuweza kuimarika.

“Hadi sasa hatujajua kosa lililosababisha mbunge huyo akamatwe na polisi,lakini yote tunamwachia Mungu” alisema Sokombi.

Bulaya alikamatwa juzi na polisi wilayani Tarime baada ya kumalizika kwa mkutano wa hadhara wa Mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko ambapo anadaiwa kuongea maneno ya uchochezi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles