22.2 C
Dar es Salaam
Monday, October 18, 2021

BUKOBA WAKUSANYA LITA MILIONI 98 ZA MAZIWA

Na Renatha Kipaka


 ZAIDI ya lita milioni 97.8 za maziwa zilikusanywa  kwa matumizi mbalimbali kutoka kwa wafugaji wa ng’ombe wa maziwa   kwenye wilaya nane za Mkoa wa Kagera  kwa kipindi cha mwaka 2016/017 ikilinganisha na  lita milioni 46.6   mwaka 2015/016

 Makusanyo hayo yanatokana na taratibu zilizopo katika mkoa huo   kujua zao hilo linanufaishaje jamii.

Ofisa Mifugo Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo, Colman John   alisema lengo ni kila kaya kutumia  maziwa   na wafugaji kujipatia kipato.

 Alikuwa akizungumza na wandishi wa habari   ikiwa ni maandalizi ya maadhimisho ya wiki ya maziwa kuanzia Juni  mosi mwaka huu.

 John alisema  tofauti hiyo ya ukusanyaj inatokana na   mabadiliko ya tabianchi   ambako ukame ulitawala na kusababisha kutokuwapo   maji na nyasi za kutosha.

 “Mabadiliko yanayotokea na kuonekana hapa   ni ukame uliosababishwa na ukosefu wa mvua kwa muda mrefu  na kusababisha ng’ombe kukosa lishe na maji,”alisema.

 

Alisema  mkoa huo una  ng’ombe wa maziwa wapatao 21,438 na ng’ombe wa asili 52,8632. 

”Niseme tu kwamba taarifa hizo tunazipata kuanzia ngazi ya kijiji hadi wilaya maana wao ndiyo wanaojua ni nani anafuga na nani anayekamua maziwa kiasi gani,” alisema.

 Meneja wa Kiwanda cha Maziwa Kagera katika o Manispaa ya Bukoba,  Samwel John alisema kwa sasa upatikakanaji wa maziwa kwenye kiwanda hicho ni wa kiwango cha chini ikizingatiwa hukusanya lita 200-300 za maziwa kwa siku   ndani ya manispaa hiyo.

 Alisema awali kiwanda hicho kilikuwa kinapata maziwa kutoka maeneo mbalimbali ya wilaya lakini kwa sasa hayapatikani kwa wingi. 

“Kama sisi hapa tunazalisha maziwa aina tatu, maziwa fresh, yogati na mtindi kwa uwiano wa lita 150 ni fresh, lita 100 ni yogati na lita 50 matumizi ya watu majumbani,” alisema John.

Naye Methodi Karikira, mtumiaji wa maziwa klra siku na mkazi wa Manispaa ya Bukoba, alisema   ulipotokea ukame maziwa yalikuwa ya shida kupatikana hata katika familia.

Alisema   sababu nyingine ya upungufu wa maziwa ni ardhi kutokuwa na madini ya chumvi na kufanya wafugaji kuwapa ng’ombe wao chumvi ya kawaida kwa wingi.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
162,220FollowersFollow
521,000SubscribersSubscribe

Latest Articles