26.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, October 27, 2021

BUHARI AOMBWA ACHUKUE LIKIZO YA MATIBABU

ABUJA, NIGERIA


KUNDI la watu mashuhuri nchini hapa, limemtaka Rais Muhammadu Buhari kuchukua likizo ya matibabu kutokana na wasiwasi kuhusu hali yake ya afya.

Kwa mujibu wa kundi hilo la watu 13 mashuhuri, hatua ya Buhari kutohudhuria mikutano miwili ya Baraza la Mawaziri inaashiria kuzorota kwa afya yake.

Kundi hilo linashirikisha wanaharakati wenye ushawishi akiwamo wakili Femi Falana, mchanganuzi wa masuala ya kisiasa, Jibrin Ibrahim na Kiongozi wa Shirika la Transparence International tawi la Nigeria, Anwal Musa Rafsanjani.

Buhari (74) alichukua wiki saba za likizo ya matibabu Januari, mwaka huu na kusafiri hadi nchini Uingereza.

Wakati aliporudi nyumbani Machi, mwaka huu, alisema kuwa hajawahi kuwa mgonjwa kupita kiasi maishani mwake.

Buhari hajatangaza kile anachoumwa, lakini aligusia tu kuwa aliongezewa damu.

Wasaidizi wa Buhari hawajatoa tamko lolote kuhusu taarifa hiyo.

Wiki iliyopita, msemaji wa Rais Buhari, Garba Shehu, alisema Buhari alikuwa akifanya mambo polepole, huku akiendelea kupona kufuatia kipindi kirefu cha matibabu nchini Uingereza.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
163,388FollowersFollow
522,000SubscribersSubscribe

Latest Articles