25 C
Dar es Salaam
Sunday, October 6, 2024

Contact us: [email protected]

Buhari akabiliwa na ushindani mkali urais Nigeria

LAGOS, NIGERIA

RAIS Muhammadu Buhari anakabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa kiongozi wa upinzani, Atiku Abubakar katika kampeni zinazoendelea sehemu mbalimbali za nchi kuelekea uchaguzi wa Februari 16.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari, kadiri siku zinavyozidi kwenda katika kampeni hizo, inaonekana Rais Buhari wa Chama cha APC anakabiliwa na ushindani mkali kutoka kwa Abubakar – mgombea wa Chama cha People’s Democratic Party (PDP) aliyekuwa Makamu wa Rais.

Uchaguzi huo mkuu unawakutanisha wagombea 60 wa urais, japo wengine nafasi yao ya kushinda ni ndogo sana.

Mali na ushawishi wa kisiasa kati ya vyama vikuu vyenye ushawishi na ushindani mkubwa ndio vigezo vikubwa katika siasa za hapa, nchi yenye utajiri mkubwa wa mafuta na idadi kubwa ya watu barani Afrika.

Mwishoni mwa wiki, wakati wa mkutano wa kisiasa mjini hapa, Rais Buhari aliwaambia maelfu ya wafuasi wake kwamba ataendelea kutimiza ahadi alizotoa wakati wa uchaguzi wa mwaka 2015 ambazo ni kupambana na ufisadi, kuimarisha ukuaji wa uchumi na kuimarisha usalama.

Hata hivyo, Serikali yake inakabiliwa na changamoto kubwa ya usalama kutoka kwa makundi ya wapiganaji wa Boko Haram na Islamic State huku hali ya umasikini ikiendelea kuongezeka.

Hata hivyo sera hizo zinapingwa vikali na wapinzani wake ambao katika kampeni zao wanasema Serikali imeshindwa kukabiliana na ufisadi na kuwalenga tu maadui wake, huku ikikosa kukabiliana na madai yanayohusu washirika wake katika vita dhidi ya ufisadi.

Amnesty International na watetezi wa haki za binadamu nao wanashutumu jeshi la hapa kwa ukandamizaji wa haki za kibinadamu, ikiwemo mauaji ya waandamanaji ingawa  jeshi linatetea matumizi ya nguvu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles