23.2 C
Dar es Salaam
Monday, February 6, 2023

Contact us: [email protected]

BROWN AMFANYIA ‘BIRTHDAY’ KRISTINA

GEORGIA, MAREKANI


MSANII wa muziki wa hip hop nchini Marekani, Bobby Brown, juzi alifanya sherehe ya kuzaliwa kwa mtoto wake, Kristina Brown ambaye alipoteza maisha Julai 26, mwaka 2015.

Mrembo huyo juzi alikuwa anatimiza miaka 24, hivyo baba yake aliamua kumfanyia sherehe kama sehemu ya kumkumbuka huku akiweka picha mbalimbali kwenye mitandao ya kijamii za enzi za uhai wake.

Hata hivyo, msanii huyo aliweka picha nyingine za mke wake marehemu, Whitney Houston, ambaye alifariki dunia Februari 11, mwaka 2012 na kumwachia mtoto mmoja Kristina Brown.

“Kristina alikuwa kama malaika kwangu, siku kama ya leo (juzi), tungekuwa pamoja na kusherehekea siku yake ya kuzaliwa kwa kufikisha miaka 24, lakini ametangulia mbele ya haki ninaamini ipo siku tutakuja kukutana,” aliandika Brown.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,471FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles