31.7 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

BROOKINGS INSTITUTE: AFRIKA IENDELEZE MAHUSIANO KIBIASHARA 

Na GEORGE MSHANA


SERA ya Marekani kwa Afrika baada ya kuchaguliwa kwa Donald Trump kuwa Rais wa Marekani, bado ina nguvu baada ya kuungwa mkono na marais watatu waliomtangulia yaani Bill Clinton, George W. Bush na Barack Obama na kupitishwa na bunge la Congress.

Taasisi ya Brookings Institute ya Marekani inasema kwenye kongamano kuwa  wanatarajia kwamba misaada kwa Afrika kupitia makubaliano yaliyopitishwa na Congress itaendelea kutolewa hata katika utawala huu wa Donald Trump.

Katika makubaliano hayo, iliamuliwa kwamba Afrika ina fursa za kiuchumi na kiuwekezaji ambazo Marekani wangependa kuzitumia na kuja kufanya biashara na kuwekeza.

Katika miongo miwili iliyopita, Bunge la Congress la Marekani lilipitisha sheria inayoitwa African Growth and Opportunity Act (AGOA) na pia walipitisha mpango wa dharura wa rais wa kupunguza kasi ya maambukizi ya ugonjwa wa ukimwi (PEPFAR) na kuanzisha Millennium Challenge Corporation (MCC) na hivi karibuni wamepitisha sheria ya Power Afrika ambapo Marekani itatoa ufadhili wa miradi ya umeme kwa nchi saba za Afrika ikiwemo Tanzania.

Sheria ya Usalama wa chakula (Food Security Act) ilianzishwa ili kutoa misaada ya chakula kwa nchi zenye uhitaji wa chakula.

“Tunaamini kwamba Rais Donald Trump ataendelea kutoa misaada kwa Afrika kupitia hii mipango ambayo ilianzishwa na watangulizi wake yenye lengo la kulisaidia bara la Afrika kupata maendeleo endelevu ya kiuchumi.

 “Hata hivyo, ni matumaini yetu kwamba Rais Donald Trump ataipa Afrika kipaumbele katika kuipatia misaada na uwekezaji ili iweze kuwa na maendeleo endelevu ya kiuchumi. Pia na kufanya nayo biashara kupitia AGOA ambapo bidhaa za nguo zinauzwa kwa bei nafuu na wafanyabiashara wetu wa Tanzania waitumie fursa hii vizuri ili kuweza kujiimarisha kiuchumi,” anasema Whitney Schneidman, kutoka taasisi ya kimataifa ya uchumi na maendeleo ya Brookings.

Manufaa yaliyopatikana kutokana na AGOA yamekuwa ndiyo nguzo kuu ya mahusiano kati ya Marekani na Afrika. Hii imesababisha biashara na uwekezaji kuwa kipaumbele katika sera za Marekani barani Afrika. AGOA imewapa moyo wanawake wa Afrika kufanya biashara na Marekani kupitia kutengeneza bidhaa ambazo zinakubaliwa na Marekani katika mpango wake wa AGOA, hasa wakati wa utawala wa Rais Obama ambapo makampuni ya Afrika yalisaidiwa kuuza bidhaa zao kupitia mpango wa AGOA,” anasema Whitney.

Katika miaka kumi iliyopita, Umoja wa Ulaya umetaka kutekeleza makubaliano ya kiuchumi yanayoitwa ‘Economic Parnership Agreements’ katika bara la Afrika ambapo unazitaka Serikali za nchi za Afrika kukubali bidhaa za Ulaya ziingie bila kulipiwa ushuru na za Afrika ziingie Ulaya bila kulipiwa Ushuru.  

“Ni muhimu kubadili mwelekeo wa ushirikiano kati ya Marekani na Afrika kutoka kwa mfadhili na mpokea misaada na kuwa na faida kwa pande zote mbili (yaani mutual benefit). Misaada mingi kutoka Marekani ni msaada na si mkopo. Wakati nchi nyingi za Afrika zina uwezo wa kuamua ni miradi ipi Marekani watawekeza. Kwa mfano, Millennium Challenge Corporation (MCC), ambayo inaratibu misaada yake kwa majadiliano na timu ya wataalamu kutoka nchi inayopokea misaada. Bado hatujajua kwamba utawala wa Donald Trump utaweza kuendeleza makubaliano haya na kuendelea kujenga urafiki na mahusiano ya kibiashara na kiuwekezaji kati ya Marekani na Afrika,” anasema Whitney.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles