Britney Spears atikisa chati za iTunes

0
957
Britney Spears

NEW YORK, MAREKANI 

STAA wa muziki na filamu nchini Marekani, Britney Spears, ameandika historia mpya kwenye chati za iTunes baada ya albamu yake ya ‘Glory’ kushika nafasi ya kwanza.

Albamu hiyo iliachiwa tangu 2016, lakini mwishoni mwa wiki iliopita albamu hiyo ilitangazwa kushika nafasi ya kwanza kwa mara ya kwanza.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, mrembo huyo mwenye umri wa miaka 38, aliposti video yake akionesha chati hizo pamoja na kuwashukuru mashabiki zake.

“Helo mashabiki zangu, nitumie nafasi hii kushukuru kwa albamu yangu kushika nafasi ya kwanza kwenye chati za iTunes, sikuwa na wazo kama litatokea hili, lakini hii yote ni kutokana na uwepo wenu mashabiki, naweza kusema hii ni siku yangu bora ambayo haijawahi kutokea,” aliandika mrembo huyo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here