23.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

BRAZIL WAPOKEA MIILI YA WACHEZAJI WA CHAPECOENSE

blankets-bearing-the-crest-of-brazilian-soccer-team-chapecoense-are-placed-on-coffins-holding-the-re

CHAPECO, BRAZIL

MIILI ya watu 71 ambao walipata ajali ya ndege nchini Colombia Jumatatu wiki hii, imerudishwa kwao kwa ajili ya mazishi, huku ikiwa pamoja na wachezaji wa timu ya Chapecoense ambao wamepoteza maisha.

Wachezaji hao walikwenda nchini Colombia kwa ajili ya mchezo wa kwanza wa fainali ya Copa Sudamericana dhidi ya Atletico Nacional, lakini walipoteza maisha wachezaji 19, huku watatu wakitoka hai.

Tangu tukio hilo litokee, mashabiki wa klabu hiyo ya Chapecoense na Atletico Nacional, waliungana kwa ajili ya kuombeleza msiba huo mzito kwa upande wa soka Brazil na duniani kwa ujumla.

Miili ya wachezaji hao pamoja na viongozi, iliwasili jana nchini Brazil kutokea nchini Colombia kwa ajili ya mazishi, maelfu ya mashabiki na wadau mbalimbali wa soka walijitokeza katika kiwanja cha Chapecoense kwa ajili ya kutoa heshima za mwisho.

Inadaiwa kwamba mashabiki zaidi ya 100,000 walijitokeza kwa ajili ya kuwaaga mashujaa wao, huku huzuni ikitawala kwenye viwanja hivyo.

Mapokezi ya miili hiyo ya wachezaji wa soka pamoja na viongozi yaliongozwa na rais wa nchi hiyo ya Brazil, Michel Temer, katika uwanja wa ndege.

Hata hivyo, rais huyo alishindwa kwenda katika uwanja wa Chapecoense kutokana na kuhofia maandamano ya mashabiki hao wa soka, lakini ndege mbili za kijeshi ziliwasili kwenye uwanja huo kwa ajili ya usalama.

Katika ajali hiyo watu 64 ni raia wa nchini Brazil ambao wamepoteza maisha, huku watano wakiwa raia wa nchini Bolivia, Venezuela na Paraguay.

Chanzo cha ajali hiyo hadi sasa hakijajulikana rasmi, lakini kuna taarifa kwa watu wa anga zinasema kuwa, rubani wa ndege hiyo alitoa taarifa juu ya tatizo la umeme, hivyo aliweza kumwaga mafuta kwa kuzuia mlipuko.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles