29.7 C
Dar es Salaam
Monday, October 2, 2023

Contact us: [email protected]

Brazil wajipa matumaini bila Neymar

RIO, BRAZIL

BAADA ya timu ya taifa Brazil kuanza vizuri kwenye michuano ya Copa America, nahodha wa timu hiyo Dani Alves, ameweka wazi kuwa watakuja kufanya vizuri bila ya staa wao Neymar Jr.

Michuano hiyo ambayo inaendelea nchini humo, katika mchezo wa ufunguzi Brazil ilifanikiwa kufanya vizuri kwa kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Bolivia, hivyo kuwapa imani mashabiki zao.

Neymar ni mmoja kati ya wachezaji ambao walikuwa wanapewa nafasi kubwa ya kufanya vizuri kwenye michuano hiyo, hatimaye mchezaji huyo atakuwa nje hadi mwisho wa mashindano kutokana na kuchanika enka wakati wa mchezo wa mwisho wa maandalizi.

Kuumia kwake kumewapa wasiwasi mashabiki wa timu hiyo, lakini Alves amesisitiza bila ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27, wataweza kuipeperusha bendera yao vizuri kwenye ardhi ya nyumbani.

“Ninaamini kila wakati ambao wachezaji tunakuja kuvaa jezi ya timu ya taifa lazima tuhakikishe tunathibitisha thamani ya taifa, bila ya kujali nani yupo na nani hayupo, ila waliopo lazima wahakikishe wanatetea historia ya timu.

“Lakini ukiwa na kikosi ambacho ndani yake yupo Neymar unakuwa na nguvu zaidi, ila haimaanishi bila ya yeye hatuwezi kufanya lolote.

“Kikubwa kinachotakiwa baada ya kuwa na hali kama hiyo ni lazima kila mmoja aongeze nguvu zaidi ya awali ili kuziba nafasi ya mchezaji ambaye hayupo. Kila mchezaji jukumu lake limebaki vile vile kwa ajili ya kulipigania taifa,” alisema nahodha huyo.

Miongoni mwa wachezaji wa timu ya taifa ya Brazil ambao wamecheza michezo mingi ya timu hiyo ni pamoja na Cafu ambaye alicheza jumla ya michezo 142 akifuatiwa na Roberto Carlos michezo 125, wakati huo Alves hadi sasa akiwa amecheza michezo 110, lakini bado anaamini atakuwa kwenye kitakacho kwenda kushiriki Kombe la Dunia nchini Qatar mwaka 2022 bila ya kujali umri wake wa miaka 36 alionao sasa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles