23.7 C
Dar es Salaam
Sunday, August 14, 2022

Brad Pitt, Angelina Jolie wawaacha njia panda mashabiki wao

brad-pitt-angelina-jolie

WANAPOACHANA watu mashuhuri mengi hutokea, hasa kwa mashabiki wao waliokuwa wakifuatilia kila kilichofanywa na watu hao mashuhuri na wakati mwingine huwa watetezi kwa lolote baya lifanywalo na watu hao, lakini huwa ngumu kuonyesha mapenzi yao kwa mmoja kama watu hao watatengana.

Hilo ndilo linaloonekana kutokea kwa mashabiki wakubwa; Angelina Jolie na Brad Pitt baada ya Jolie kuwasilisha hati ya kudai talaka ya ndoa yao yenye miaka miwili sasa.

Utata wa wacheza filamu hao maarufu duniani, Angelina Jolie na Brad Pitt,  ulianza kwa kutofautiana kwao katika masuala mengi likiwemo la malezi ya watoto wao sita.

Suala hilo limechukua sura mpya baada ya Brad Pitt (52) kukasirishwa na tabia ya Jolie ya kuweka wazi maisha ya watoto wao, akidai ni jambo la hatari kwa watoto hao.

Wapenzi hao wenye miaka miwili  ya ndoa, uhusiano wao wa kimapenzi ulianza tangu walipokutana katika filamu ya Mr. & Mrs. Smith, waliyocheza mwaka 2003.

Ugomvi wa wawili hao wanaodaiwa kutengana, ulianza baada ya Jolie kutokukubaliana na namna ambavyo Pitt anavyowalea watoto wao, jambo lililomkera Pitt kwani hakufurahishwa na kauli za mwandani wake huyo akidai kauli hizo zinahatarisha usalama wa watoto hao.

Jolie aliyenoga katika filamu ya ‘Maleficent’, aliandika nyaraka za kuomba talaka na kuwasilisha September 15, mwaka huu ili asitishe ndoa yao ya miaka miwili na mwanamume huyo, huku akitaka aishi na watoto wao wote lakini anataka kuwe na uhuru kwa Pitt kwenda kuwasalimia.

Wadau mbalimbali wa masuala ya mahusiano wanasema Pitt hataki kuharakisha kuachana kutokana na kudhania kwamba watoto hao sita; Maddox (15), Pax (12), Zahara (11), Shiloh (10), na mapacha Knox na Vivienne ambao wana miaka nane, watawatengenezea maisha ya kutengana.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,695FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles