BOW WOW ADAI ANATENGWA

0
1036

CALFORNIA, MAREKANI


RAPA Shad Moss, maarufu kwa jina la Bow Wow, ametumia ukurasa wake wa Twitter na kudai kwamba, amekuwa mmoja kati ya wasanii ambao wanatengwa na kuchukiwa.

Staa huyo ambaye alianza kuwa na jina kubwa tangu akiwa na umri mdogo, amesisitiza kwamba, maisha yake kwa sasa yamekuwa na changamoto nyingi.

“Wala sijali, vyombo vya habari vimekuwa vikinisema vibaya, nimekuwa miongoni mwa watu wanaochukiwa sana, kila msichana ambaye nilimpa moyo wangu aliniangusha, baba yangu ni mlevi na sasa ni mgonjwa, mchumba wangu alipoteza mtoto kwa ajili ya mimba kuharibika, nimekuwa nikiguswa na kila kitu, akili yangu haipo sawa kabisa, naumia sana,” aliandika Bow Wow.

Hata hivyo, kabla ya mashabiki wake kuanza kujibu ujumbe huo, aliamua kufuta Twitt hiyo, lakini baada ya muda aliendelea kuandika ujumbe mwingine kwa kumwelezea mpenzi wake, Kiyomi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here