28.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

BOT YATANGAZA BENKI YA FBME KUFILISIKA

Baadhi ya wateja wa Benki ya FBME wakisoma tangazo lililowekwa na Benki Kuu ya Tanzania (BOT) la benki hiyo kufutiwa leseni ya biashara,Dar es Salaam jana.Picha na John Dande

 

Na MWANDISHI WETU,

BENKI Kuu ya Tanzania (BOT), imesimamisha shughuli zote za Benki ya  FBME na kufuta leseni yake ya kufanya shughuli za kibenki.

Hatua hiyo ya BOT, imetokana na Taasisi ya Marekani inayopambana na uhalifu wa kifedha (FinCEN) kutoa uamuzi wa kuifungia benki hiyo  kutumia mfumo wa kibenki wa Marekani.

Hatua hiyo ilitokana na notisi iliyotolewa Julai 15,2014  na Taasisi ya Marekani inayopambana na uhalifu wa kifedha  iliyoituhumu FBME kuwa ni taasisi inayojihusisha na biashara ya utakatishaji wa fedha haramu .

Pia hatua ya Benki Kuu ya Cyprus kuliweka tawi la FBME lililopo nchini Cyprus chini ya uangalizi maalumu, imesababisha BOT kuifungia benki hiyo.

 FBME haikukubaliana na uamuzi huo na kuamua kufungua kesi katika mahakama huko Marekani, wakiiomba mahakama kutengua uamuzi wa FinCEN.

Hata hivyo, April 14,  mwaka huu mahakama ilitoa uamuzi ambao unairuhusu FinCEN kuendelea na utekelezaji wa uamuzi wake wa mwisho  ambao unaifungia benki ya FBME kutumia mfumo wa kibenki wa Marekani.

Taarifa ya BOT, inaeleza  uamuzi huo unaongeza athari kwa kiwango kikubwa katika uendeshaji wa FBME kwa kuwa haitaweza tena kufanya miamala ya kibenki ya kimataifa, hivyo itashindwa kutoa huduma muhimu kwa wateja wake kwa mujibu wa leseni waliyopewa.

Kwa kuzingatia athari zinazotokana na uamuzi wa mwisho wa FinCEN, kwa mamlaka iliyopewa chini ya kifungu cha 58(2)a, 11(3)(i), 61(1) na 41(a) vya Sheria ya Mabenki na taasisi za fedha ya mwaka 2006  BoT iliiweka chini ya usimamizi maalumu benki ya FBME.

Bodi ya bima ya amana kuwa mfilisi imesema kuanzia  mei 8 mwaka huu  na kwa wale wenye amana, wadai na wadaiwa kuwa wawe wavumilivu wakati mfilisi akiandaa utaratibu wa kushughulikia stahiki zao.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles