22.8 C
Dar es Salaam
Saturday, June 3, 2023

Contact us: [email protected]

BoT yaondoa masharti ya kufanya biashara ya Wakala wa benki

Na Ramadhan Hassan, Dodoma

BENKI Kuu ya Tanzania (BoT) imeweka hatua tano za kisera ili kuongeza upatikanaji wa mikopo kwa sekta binafsi na kupunguza viwango vya riba ikiwemo kuondoa sharti la uzoefu wa kufanya biashara kwa angalau miezi 18 kwa waombaji wa biashara ya wakala wa benki.

Hiyo ina maana kuwa sasa muombaji wa biashara ya wakala wa benki atatakiwa kuwa na Kitambulisho cha Taifa au namba ya (NIDA).

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Jumanne Julai 27, jijini Dodoma, Gavana wa BoT, Prof. Florens Luoga amezitaja hatua hizo kuwa ni pamoja na kupunguza kiwango cha sehemu ya amana za mabenki kinachotakiwa kuwekwa benki kuu.

“Nafuu hii itatolewa kwa benki itakayotoa mikopo kwa sekta ya kilimo kulingana na kiasi cha mkopo kitakachotolewa. Benki itakayonufaika itatakiwa kutoa kwa sekta ya kilimo kwa riba kwa riba isiyozidi asilimia 10 kwa mwaka,” amesema.

Ameitaja hatua nyingine ni kupunguza masharti ya usajili wa mawakala wa benki kwa BoT kuondoa sharti la uzoefu wa kufanya biashara kwa angalau miezi 18 kwa waombaji wa biashara ya wakala wa benki.

Amesema badala yake waombaji wa biashara ya wakala wa benki watatakiwa kuwa na Kitambulisho cha Taifa au namba ya Nida.

Ameitaja hatua nyingine ni ukomo wa riba kwenye akaunti za Makampuni ya watoa huduma za fedha kwa njia ya simu za mkononi.

Pia, kuanzishwa kwa Mfuko Maalum wa kukopesha Mabenki na Taasisi za kifedha ili ziweze kukopesha sekta binafsi.

Prof. Luoga ameitaja hatua nyingine ni kupunguza kiwango cha mtaji kinachotakiwa kuwekwa na benki za biashara kwa ajili ya kuweza kutoa mikopo.

“Hatua hizi za kisera zimechukuliwa kwa kwa mujibu wa sheria ya Benki kuu sura ya 197 na Sheria ya Mifumo wa malipo ya Taifa sura 437, Benki kuu itatoa mwongozo wa namna ya utekelezaji wa hatua hizi za kibenki,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,270FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles