23.2 C
Dar es Salaam
Thursday, August 11, 2022

Bosi Simba aibua sekeseke mazoezini

Zainab Iddy -Dar es salaam

INAPENDEKEZA ukiiita ‘surprise’, baada ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa Simba, Senzo Mazingiza jana kuibuka ghafla katika mazoezi ya timu hiyo yaliyofanyikwa Viwanja vya Gymkhana, Dar  es Salaam.

Kitendo cha bosi huyo kutokea mazoezini ghafla kilisababisha wachezaji wa timu hiyo kupatwa na mshtuko kwakua hawakutegemea.

Mazoezi ya timu hiyo yalikuwa yakiongozwa na Kocha Msaidizi, Denis Kitambi na yule wa viungo, Adel Zrane.

Ishu yenyewe ilivyokuwa, wakati wachezaji wa timu hiyo wakiendelea na mazoezi, ghafla Mazingiza alitokea na moja kwa moja alikwenda kwa meneja wa kikosi hicho, Patrick Rweyemamu.

Mazingiza alimuhoji meneja sababu za kutoonekana mazoezini kwa baadhi ya wachezaji wa timu hiyo.

Meneja Rweyemamu alimjibu kwa kueleza kuwa anazo taarifa za Erasto Nyoni, Miraji Athuman na Francis Kahata kwamba hawakushiriki mazoezi hayo kutokana na kuomba udhuru.

Wakati Mazingiza akizungumza na meneja, nyota wa timu hiyo, Jonas Mkude, Clatous Chama na Pascal Wawa walikuwa wamejenga kijiwe wanazungumza lakini  baada ya kumuona bosi wao huyo haraka haraka walikatisha na kujiunga na wenzao, kitendo kilichotafsirika walipatwa na ubariki.

Katika mazoezi hayo ambayo yalianza saa nne asubuhi na kumalizika saa sita, wachezaji wa timu hiyo walianza program ya siku kwa kukimbia, kisha wakafanya mazoezi ya viungo kabla ya kuhitimisha kwa kucheza mechi kwa mafungu mafungu iliyotumia dakika 15 kila moja.

Wakati huo huo, Senzo alishindwa kuweka wazi mustakabali wa Kocha  Mkuu wa timu hiyo, Patrick Aussems ambaye anahusishwa kuachana na Wekundu hao wakati wowote kuanzia sasa.

Mazingiza alisema hawezi kuzungumzia hatma ya kocha wao huyo kwakua si wakati sahihi wa kufanya hivyo.

“Nimekuja mara moja kuangalia kinachoendelea, lakini sipo katika nafasi nzuri ya kuzungumzia suala la kocha na taarifa zinazoendea kuzagaa.

“Naomba msubiri kuna mambo yakishawekwa sawa nitaita vyombo vya habari na kuweka wazi kila kitu,”alisema raia  huyo wa Afrika Kusini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,411FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles