23 C
Dar es Salaam
Monday, August 15, 2022

Bosi mpya Tony Elumelu aanza majukumu yake

Mwandishi Wetu

Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Taasisi ya Tony Elumelu ya nchini Nigeria, Ifeyinwa Ugochukwu, ameanza majukumu yake mapya kuanzia Aprili 1, mwaka huu.

Ifeyinwa anakuwa Mkurugenzi Mtendaji wa tatu na wa kwanza kwa Afrika kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Tony Elumelu, ambapo kabla ya kuchukua nafasi hiyo aliwahi kuwa Mkurugenzi wa Ushirikiano na Tahmini wa taasisi hiyo.

Desemba mwaka jana Taasisi ya Tony Elumelu ambayo inafanya kazi ya kuwawezesha wajasiriamali wa Kiafrika, ilitangaza uteuzi mpya wa Ifeyinwa kama Mkurugenzi Mtendaji nafasi ambayo ilikuwa ikishikiwa na mtangulizi wake Parminder Vir, ambaye kwa sasa anakuwa Mkurugenzi wa Bodi ya Ushauri wa Tony Elumelu.

Akizungumzia majukumu yake hayo mapya, Ifeyinwa amesema atazingatia kuongeza umuhimu wa Programu ya Uwekezaji wa Tony Elumelu ya Dola milioni 100 kwa kipindi cha miaka 10 na kuimarisha mahusiano kati ya Afrika na mfumo wa kimataifa wa ujasiriamali, kuwawezesha wajasiriamali wa Afrika na matokeo ya kujenga ajira na mali juu ya bara.

“Katika kipindi cha miaka miwili nimekuwa katika kutoa uzoefu nikiwa Mkurugenzi wa Ushirikiano na Tathmini kabla ya kupata nafasi mpya ya kuongoza taasisi hii,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,800FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles