27.5 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Bosco Ntaganda aanza kula baada ya kugoma wiki mbili ICC

Bosco Ntaganda
Bosco Ntaganda

HAGUE, UHOLANZI

ALIYEKUWA kiongozi wa waasi katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Bosco Ntaganda, ameanza kula baada ya kugoma kwa takribani wiki mbili katika kizuizi chake kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) mjini Hague, Shirika la Habari Ufaransa (AFP) linaripoti.

Ntaganza anayejulikana kwa jina la utani ‘The Terminator’ kutokana na shughuli zake katika uwanja wa vita nchini Congo, aligoma kula kulalamikia hali inayomkabili kizuizini, ikiwemo kuzuiwa kutembelewa na familia yake.

AFP imemnukuu wakili wake, Stephane Bourgon, aliyesema kuwa bwana vita huyo wa zamani ambaye anakabiliwa na mashtaka ya uhalifu wa kivita ameanza tena kula.

“Iwapo kila kitu kitakwenda sawa, mkewe atafika The Hague kuanzia Alhamisi na ataweza kumuona Ntaganda kwa kiwango fulani cha faragha, kitakachokidhi matarajio yake,” aliongeza wakili wake.

Mwaka jana, Ntaganda alikana mashtaka 18 yanayomkabili – ikiwemo mauaji, kuwasajili watoto katika jeshi na kuwatumia wanawake kama watumwa wa ngono

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles