Boomplay yasheherekea Siku ya Wanawake na wasanii wa kike

0
1256

Mwandishi Wetu

Katika kusherehekea Siku ya Wanawake Duniani, Aplikesheni maarufu Afrika ya kusikiliza na kupakua nyimbo mtandaoni ya Boomplay, imesherekea Siku ya Wanawake Duniani kwa ni nambari moja kwa huduma ya kusikilizana kupakua muziki barani Afrika, inasherehekea Siku Ya Wanawake Duniani mwaka huu kwa kuweka mwonekano tofauti uliopambwa na picha za wasanii wanawake.

Meneja Mahusiano wa Kampuni ya Boomplay, Tosin Sorinola, amesema
hatua hiyo pia ni katika kampeni mpya ya Boom Queens.

“Boomplay itakuwa na muonekano wa tofauti hasa katika Siku Ya Wanawake duniani Machi 8, lengo likiwa ni kuonesha na kukuza kazi za wanawake katika muziki.

“App itapambwa na nyimbo, albamu pamoja na orodha (playlist) za wanawake katika vipengele vyote kwenye ukurasa wa kwanza,” amesema.

Akizungumzia kampeni ya Boom Queens, amesema itatoa fursa ya kukuza mauzo ya kazi za wanawake ambapo nyimbo zao zitakuwepo kwenye playlist ya Boom Queens.

“Playlist hiyo itakuwa na nyimbo za wasanii bora wa kike, aidha majadiliano juu ya usawa wa kijinsia ni moja ya mambo ambayo ni muhimu kwetu kama jukwaa lenye nia kubwa ya kukuza wanawake katika muziki, katika njia nje na kadri iwezekanavyo.

“Kampeni hii siyo kwa mara moja tu, ni endelevu, na hili litadhihirishwa katika shughuli zetu za kila siku,” amesema.

Pamoja na mambo mengine, amesema katika mwezi huu wa kuadhimisha Siku Ya Wanawake Duniani, watumiaji wa Boomplay kupitia simu zao za Android na iOS watapata fursa ya kujishindia simu mpya ya iPhone XS na zawadi nyingine katika nchi za Tanzania, Kenya, Nigeria na Ghana.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here