26.8 C
Dar es Salaam
Saturday, September 7, 2024

Contact us: [email protected]

Boniventura: Tuitumie mitandao ya kijamii kujiendeleza kielimu

hakielimu-sept26-2015NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM

MA F A N I K I O na matokeo mazuri ya elimu kwa wanafunzi yanatokana na juhudi za mwalimu na mzazi kwa kumjengea mtoto mazingira mazuri ya kujifunzia.

Kutokana na hali hiyo, zipo shule mbalimbali ambazo walimu pamoja na wazazi wameungana kwa pamoja kuhakikisha wanawasaidia watoto wao kwa lengo la kuwapatia elimu bora yenye manufaa katika jamii.

Shule ya Sekondari ya Victor iliyopo Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani, imekuwa mstari wa mbele kuhakikisha wanafunzi wao wanawajengea mazingira rafiki ya kujifunzia.

Kaimu Mkurugenzi wa Haki Elimu, Godfrey Boniventura, hivi majuzi alikuwa mgeni rasmi katika mahafali ya nane ya shule hiyo, ambapo pamoja na mambo mengine alisema miundombinu na mazingira ya shule vimemvutia.

Anasema anaamini kwa mazingira aliyoyakuta shuleni hapo, itakuwa inafanya vizuri katika matokeo yake ya kila
mwaka ya mitihani ya taifa. Boniventura anasema bila ya wataalamu kuutumia utaalamu wao, hali ya maendeleo katika eneo husika haitakuwapo, ili pawepo na maendeleo ya elimu, kilimo,uchumi au mambo mengi ambayo
yanaweza kuliletea taifa, kipato, inatakiwa wataalamu na wasomi kutumia elimu yao ili yapatikane maendeleo sehemu husika.

“Ili tuwe na maendeleo ya haraka, inatakiwa wataalamu wetu na wasomi watumie utaalamu wao katika kuliletea taifa maendeleo,” anasema.

Boniventura anawataka wahitimu wajiepushe na tabia ya kuitumia mitandao ya kijamii kwa mambo yasiofaa, badala yake kuhakikisha wanaitumia kwa ajili ya kujifunza kujua mambo yanayotokea duniani.

Anasema miundombinu mizuri ndio chachu ya mafanikio katika shule yoyote katika kuongeza ufaulu kila mwaka katika mtihani wa taifa.

Anaipongeza shule hiyo kwa kutambua michango ambayo inatolewa na walimu wao na kuamua kuwapa motisha ili
kuongeza mafanikio ya kielimu.

“Ni kweli bila ya kutoa motisha kwa walimu na wanafunzi msitegemee shule inaweza kufanya vizuri, mitihani yake hata ile ya kawaida, kinachotakiwa ni kuwajali walimu na wanafunzi na si kujali kupokea ada na kushindwa kuutambua mchango ambao unatolewa na walimu,” anasema Boniventura.

Kwa upande wake MkurugenziMtendaji wa shule hiyo, Thadei Mutembei, anasema mikakati ya shule yao ni kuhakikisha kila mwaka wanafanya vizuri katika mitihani ya kitaifa.

Anasema uongozi wa shule umekuwa ukitoa motisha kwa walimu, wanafunzi na wazazi hivyo, imesaidia shule hiyo kila mwaka kuingia 10 bora katika Mkoa wa Pwani.

Mutembei anasema mfumo huo utaendelea kila mwaka ili kuweza kutengeneza matunda mazuri yenye manufaa kwa jamii na taifa kwa ujumla.

Naye Mkuu wa shule hiyo, Christopha Segereti, anasema mkurugenzi wao ni Mtanzania mzawa, mzalendo na mpenda maendeleo hasa katika sekta ya elimu na amekuwa mwepesi kuunga mkono juhudi za serikali katika kutengeneza mazingira bora ya kufundishia na kujifunzia ili elimu bora itolewe kwa vijana.

Anasema baadhi ya Watanzania wale wenye uwezo kifedha wamekuwa wakiwapeleka watoto wao kusoma nje ya nchi kwa kuhofia aina ya elimu inayotolewa hapa nchini, lakini mkurugenzi wa shule hiyo amekuwa mstari wa mbele kubadilisha mawazo yao kwa kuanzisha shule ya St. Mathews, St. Marks, Ujenzi na baadaye Victory.

Anasema ni ukweli usiopingika kwamba elimu inayotolewa katika shule hizi ni bora na yenye kukidhi viwango vya elimu nchini.

Segereti anasema katika mahafali hayo zaidi ya wanafunzi 200 wanatarajia kumaliza elimu ya kidato cha nne, ambapo kati yao wasichana ni 127 na wavulana ni 123.

Maendeleo ya kitaaluma

Akizungumzia maendeleo ya kitaaluma, anasema mkakati wa shule hiyo ni kuona matokeo makubwa kila mwaka
yanapatikana . Anasema matokeo ya mitihani ya kidato cha pili katika kipindi cha mwaka 2012/13, na 14 wanafunzi
walifanya vizuri katika mitihani yao kwa asilimia 100 ambapo wote waliingia kidato cha tatu.

Segereti anasema kwa kidato cha nne katika kipindi cha mwaka mwaka 2012 hadi 2014 wanafunzi waliofanya mitihani walifanikiwa kufaulu ambapo wengine walienda shule za serikali na wengine shule za watu binafsi.

Motisha kwa walimu Segereti anasema kila mwalimu ambaye anafaulisha mitihani yake ya masomo, anapata motisha kama ishara ya shukrani kutoka kwa mmiliki wa shule.

“Motisha hizo ni safari za nje ya nchi, kununuliwa magari na kupatiwa kompyuta,” anasema Segereti.

Anasema motisha kwa wanafunzi ni punguzo la ada pamoja na kupatiwa vitabu vya kusoma ambavyo vinamwezesha
kufanya vizuri katika masomo yake.

Wakati wazazi hupatiwa punguzo la ada na kuna baadhi ya wanafunzi ambao wanapata motisha ya kusoma kidato cha tano bure katika shule yao ya St. Mathew iliyopo Mkuranga mkoni Pwani.

Segereti anasema mafanikio ya nidhamu katika shule hiyo imeweza kufanya vizuri ambapo hata wale watoto ambao walikuwa wameshindikana kinidhamu, hivi sasa wamekuwa vizuri hata darasani.

Kwa upande wa wahitimu, katika risala yao wameipongeza serikali kwa kutoa vitabu ambavyo wamekuwa wakivitumia na kuwasaidia katika kujiendelea kielimu.

Wanasema katika kipindi cha miaka ya nyuma kulikuwa na utitiri wa vitabu na hali hiyo ilikuwa ikiwachanganya na
kushindwa kujua kuwa ni vitabu kipi wanatakiwa kutumia kwa ajili ya kufanyia mitihani yao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles