27.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, March 21, 2023

Contact us: [email protected]

Bongo Fleva wakimbilia Afrika Kusini

10932191_1545721332379090_380810471_nNA THERESIA GASPER

IDADI kubwa ya wasanii wanaofanya muziki wa Bongo Fleva kwenda kufanyia video za nyimbo zao nchini Afrika Kusini kwa sasa imekuwa siyo kitu cha ajabu huku wengi wao wakiamini kutawafikisha kimataifa.

Hivi karibuni wasanii mbalimbali akiwemo, Mo Music na Ben Paul wametangaza kwenda kupiga picha za video zao nchini humo kwa madai kwamba watajitangaza kimataifa.

Benard Paul ‘Ben Paul’ alieleza video anayokwenda kuifanyia kazi nchini humo ni ya wimbo aliouita ‘Ningefanyaje’ aliomshirikisha msanii kutoka Kenya, Avril na Rossie M.

“Nakwenda kurekodia video ya wimbo wangu huko Afrika Kusini kwa kuwa nataka kujiweka karibu na wasanii wa kimataifa na pia kuongeza idadi ya mashabiki na marafiki katika muziki wangu,” alieleza na kuongeza:

 

“Nimeona ni vema kuwapa ladha tofauti mashabiki wangu, kwani hakuna video hata moja ambayo nimeifanyia nje ya nchi, hivyo huu ni mwanzo wa kuwapa mambo mazuri mashabiki wangu.”

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
210,784FollowersFollow
563,000SubscribersSubscribe

Latest Articles