27.1 C
Dar es Salaam
Wednesday, October 4, 2023

Contact us: [email protected]

Bondia Patrick Day afariki dunia

CHICAGO, MAREKANI

BONDIA Patrick Day wa nchini Marekani, amepoteza maisha baada ya kupigwa KO kwenye uzani wa super welterweight, mwishoni mwa wiki iliopita katika raundi ya 10 dhidi ya mpinzani wake Charles Conwell.

Pambano hilo lilipigwa Jumamosi, hivyo bondia huyo alionekana kushindwa kuendelea na pambano hilo kabla ya kukimbizwa hospitalini kutokana na hali yake kuwa mbaya.

Inadaiwa kuwa Day alipata tatizo la ubongo kuchanganyika na damu baada ya kupigwa ngumi nyingi kichwani, hivyo alipoteza fahamu kwa kipindi chote hicho hadi alipopoteza maisha juzi mchana.

Kwa upande mwingine promota wa bondia huyo, Lou DiBella alisema, “Ni ngumu kuelezea kilichotokea. Ninakosa cha kuongea, ninajua nikiwa kama promota nitaulizwa maswali mengi ambayo natakiwa kuyajibu,” alisema promota huyo.

Day kabla ya kupigwa kwa KO katika raundi ya 10, tayari alikuwa ameangushwa chini mara mbili na kisha kufanyiwa matibabu kabla ya mara ya mwisho kubebwa moja kwa moja kwenye machela na kukimbizwa hospitalini.

Bondia Conwell ambaye alishinda pambano hilo, alitumia ukurasa wake wa Instagram na kumuombea mpinzani wake Day.

“Ndugu yangu Day, sikuwa na lengo litokee jambo ili, ila kitu ambacho nilikuwa nataka kukifanya ni kutafuta ushindi, hadi sasa siamini kilichotokea na najiuliza kwa nini imetokea hivi.

“Kila wakati najikuta nikilia huku nikiifikiria familia yako na yangu pamoja na marafiki watanichukuliaje mimi kwa kitendo hiki, nakuona kila ninapotembea na ninayasikia mambo mengi ya kushangaza juu yako, nimekuwa na mawazo ya kutangaza kuachana na ngumi kutokana na kilicho tokea, lakini ndoto zako na zangu zilikuwa ni kutwaa ubingwa wa dunia,” alisema Conwell.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles