BONDIA FRANCIS CHEKA ASHIKILIWA NA POLISI

0
791

cheka

RamadhanLibenanga ,Morogoro

Bondia Francis Cheka ashikiliwa na polisi mkoani Morogoro kwa kushindwa kulipa fidia ya shilingi milioni 28 .

Bondia huyo ambaye yuko rumande sasa, anakabiliwa na kosa la kukataa kupanda ulingoni desemba 25 dhidi ya bondia Abdalha Pazi (Dulla Mbabe) .

Kwa mujibu wa Promota wake, Kaiki Siraji, alifungua kesi katika Kituo cha Polisi cha Kawe kwakuwa Cheka alimbadilikia dakika za mwisho wakati walikuwa na makubaliano kimkataba ulio kwa mujibu wa sheria za ngumi.

Hata hivyo, Bondia Cheka atapelekwa Dar es Salaam kesho akiwa chini ya ulinzi kwa ajili ya kesi hiyo katika kituo cha Kawe ambako kesi ilifunguliwa Desemba 25.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here