26.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Bomoabomoa yanukia Kariakoo

DSC_0383Na Christina Gauluhanga, DAR ES SALAAM

MANISPAA ya Ilala imetoa siku saba kwa wamiliki wa nyumba, maduka, gereji bubu, sehemu za maegesho kuhakikisha wanaondoka katika maeneo waliyovamia kabla bomoabomoa haijawakumba.

Pia imeipa Mamlaka ya Maji Safi na Taka (DAWASCO) siku saba kuhakikisha inaunganisha mabomba ya maji taka yaliyopasuka, na kuondoa kero  ya kusambaa mitaani.

Mkurugenzi wa Ilala, Isaya Mngurumi, alikuwa akizungumza   Dar es Salaam jana alipotoa tathimini ya usafi katika manispaa hiyo.

Alisema katika operesheni ya usafi iliyoanza rasmi jana  miundombinu mbalimbali imebainika kuingiliwa na kujengwa sehemu za biashara.

Baadhi ya wamiliki wa nyumba na maduka wamekwisha kupewa notisi lakini wameendelea kukaidi hivyo manispaa inatoa siku hizo  waweze kuacha maeneo hayo wazi, alisema.

Alisema changamoto hiyo imesababisha maeneo mengi kuwa machafu kutokana na viochochoro vingi kuzibwa na kujengwa maduka.

Vilevile,  maeneo mengi yamevamiwa kwa kufanywa maegesho ya magari na gereji bubu, alisema.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles