28.7 C
Dar es Salaam
Monday, October 25, 2021

BOKO HARAM WATEKA NYARA WASICHANA WENGINE

LAGOS, NIGERIA

KUNDI la kigaidi la Boko Haram, limeteka nyara makumi ya wanawake na wasichana nchini Nigeria hali ambayo imezidisha hofu miongoni mwa raia wa nchi hiyo.

Wakazi wa maeneo ya Kaskazini Mashariki mwa Nigeria, wanasema wanachama wa kundi la Boko Haram wameteka nyara wasichana na wanawake wasiopungua 22 katika mashambulizi mawili tofauti.

Shambulizi la kwanza limefanyika katika Kijiji cha Bulka kilichoko karibu na mpaka wa nchi hiyo na Cameroon ambapo wasichana 18 wamechukuliwa mateka. 

Ripoti zinasema wapiganaji wa Boko Haram pia wameshambulia kijiji cha Dumba karibu na Ziwa Chad ambako wameteka nyara wasichana wengine wanne na kuua mwanamume mmoja.

Mwaka 2014 kundi hilo la Boko Haram liliteka nyara wanafunzi 276 wa kike waliokuwa wakisoma katika shule ya Chibok, Borno, Kaskazini mwa Nigeria. Baadhi yao wasichana hao walibahatika kutoroka na wengine kukombolewa lakini hatima ya kundi kubwa la wasichana hawa bado haijulikani hadi leo hii. 

Zaidi ya watu 20,000 wameuawa katika nchi za Nigeria, Cameroon, Niger na Chad tangu kundi hilo la Kiwahabi na kigaidi lianzishe mashambulizi huko Kaskazini mwa Nigeria mwaka 2009. 

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
163,099FollowersFollow
522,000SubscribersSubscribe

Latest Articles