30.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Boisafi: CCM haitakubali upinzani wa ndani

Safina Sarwatt-Hai

WENYEKITI wa chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Kilimanjaro Patrick Boisafi amesema kuwa chama hicho hakitakuwa tayari na upinzani wa ndani ya chama hicho, na kwamba watakaobainika watachukuliwa hatua kwa mujibu kanuni na katiba chama hicho.

Boisafi ameyasema hayo wakati akipokea gari aina toyota Hilux iliyotolewa na mjumbe wa kamati ya siasa wilaya Hai Lenga Ole Sabaya kwa CCM wilaya Hai kwa ajili ya kurahisisha shughuli za chama.

“CCM haiko tayari na Upinzani ndani ya chama na kwamba watakao bainika kuendeleza fitina na chuki tutawachukulia hatua ,na kwamba CCM inataratibu zake na kanuni zake za kiutendaji hivyo ni wakati wakufanya kazi kukijenga chama na kutatua kero za wananchi,”alisema.

Amesema kuwa wanachama wanatakiwa kuachana na mambo ya ovyo ambayo hayana manufaa kwa maslahi ya chama na Taifa kwa ujumla.

“Leo hii tumepokea gari hili kwa ajili ya kufanya shughuli za chama hivyo nanyi mkaitumie kwa shughuli ya kukijenga chama na kusimamia ilani ya uchaguzi ya CCM,”alisema.

Katibu wa CCM mkoa Kilimanjaro, Jonathan Mabihya amesema kuwa gari hilo ni kwa matumizi ya chama na kwamba litatumika kwa matumizi sahihi na siyo vinginevyo.

Akizungumza wakati akikabidhi gari hilo kwa CCM, Mkuu wa wilaya Hai na mjumbe wa kamati ya siasi wilaya Lengai Ole Sabaya amesema kuwa gari hilo limenunuliwa kwenye mnada kwa sh. milion 15 na wadau pamoja serikali kama sehemu ya kukishukuru chama kwa kazi kubwa inayofanya yakukisiamia ilani ya uchaguzi.

“Tumenunua gari hili kama kukishukuru chama chetu kwa kazi nzuri inayoifanya kwa kukisimamia ilani ya uchaguzi na utekelezaji wake hivyo hatuna budi kukishukuru na kuunga mkono juhudi kubwa zinazofanywa ,”alisema.

Aidha amesema kuwa vyama vya  upinzani vimeshakufa kwa sasa na kwamba upinzani mkubwa upo ndani ya chama na  unapaswa kukemewa haraka.

“Sasa hivi vyama vya upinzani vimekufa vifo vya kawaida kabisa lakini tatizo limebaki ndani ya CCM kuna baadhi ya wanachama wanaleta majungu na  fitina ndani ya chama,na wamesahau miiko ya chama,”alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles