29.2 C
Dar es Salaam
Friday, August 19, 2022

Bodi yawatoa hofu wakulima upatikanaji mbegu za pamba

Derick Milton, Meatu

Bodi ya pamba nchini imewatoa hofu wakulima wa zao hilo wilayani Meatu mkoani Simiyu, kuhusu upatikanaji wa mbegu za zao hilo katika kuelekea msimu mpya wa kilimo ambao tayari umeanza.

Akiongea na wakulima wa pamba katika vijiji vya Isengwa na Mwandoya wilayani humo, pamoja na kamati ya mazao ya Wilaya Mkaguzi wa pamba kutoka Bodi hiyo Wilaya Jeremiah Kalissa amesema mbegu zipo za kutosha.

Kalissa amesema jumla ya kampuni sita za pamba zimepewa kazi ya kusambaza mbegu kwa wakulima, ambapo kati ya tani 2,290 zinazohitajika kwenye wilaya hiyo tani 1,850 tayari zimesambazwa kwa wakulima.

“Mbegu zipo za kutosha hakuna mkulima atakayekosa mbegu msimu huu, tumeanza kusambaza kwa haraka… hivyo niwatoe hofu juu ya hilo, pia viuatilifu navyo vitakuja kwa wakati,” amesema Kalissa.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya hiyo Dk. Joseph Chilongani ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya mazao, amewataka wakulima kuwa wakweli katika kuchukua mbegu hizo kulingana na maeneo yao ya kilimo.

“Ukibainika unafanya hivyo tutachukulia hatua kali, baadhi yenu msimu uliopita walifanya hivyo, serikali imetoa fursa kwa kila mkulima hata kama huna fedha za kununulia utapewa lakini unakopeshwa siyo bure,” amesema Dk. Chilongani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,987FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles