30 C
Dar es Salaam
Friday, January 27, 2023

Contact us: [email protected]

BODI YA WADHAMINI CUF YAWASHTAKI SAKAYA, MAFTAHA

MGOGORO ndani ya Chama cha Wananchi (CUF), umechukua sura mpya baada ya Bodi ya Wadhamini wa chama hicho, kuwasilisha maombi mahakamani wakitaka Mbunge wa Kaliua, Magdalena Sakaya na Mbunge wa Mtwara Mjini, Maftaha Nachuma wazuiliwe kwa muda kujihusisha na masuala ya uongozi pamoja na kufanya mikutano yoyote ya chama.

Wabunge hao wameshtakiwa pamoja na wenzao sita ambao ni Thomas Malima, Omari Masoud, Abdula Kambaya, Salama Masoud, Zainab Mndolwa na Jaffar Mneke.

Maombi hayo yamewasilishwa leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, chini ya hati ya dharura na yamepangwa kusikilizwa kesho mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbroad Mashauri.

Wakili wa waombaji Hashimu Mziray ameomba maombi hayo yasikikizwe upande mmoja kesho na mahakama ilikubali ombi hilo.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,063FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles