31.7 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Bodi ya ushauri TARURA yakagua ujenzi wa barabara ya Visiga -Misugusugu

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) imeanza ujenzi wa barabara ya Visiga – Zegereni- Misugusugu yenye urefu wa Km 12.5 kwa kiwango cha lami iliyopo mkoani Pwani ili kuwezesha malighafi kuingia viwandani kwa urahisi lakini pia kutoa bidhaa viwandani na kupeleka sokoni.

Akizungumza wakati wa ziara ya ukaguzi wa miradi inayofanywa na Bodi ya Ushauri ya TARURA mkoani Pwani, Meneja wa TARURA Wilaya ya Kibaha, Mhandisi Samwel Ndoveni amesema kuwa mradi huo wa ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami unalenga kuhakikisha viwanda vilivyo katika maeneo hayo vinafikika kwa urahisi kipindi chote cha mwaka.

“Barabara hii ni mkombozi kwa wananchi pamoja na wawekezaji maana lengo ni kuhakikisha barabara hii inapitika katika kipindi chote cha mwaka ili malighafi ziingie viwandani urahisi,” amesema Mhandisi Ndoveni.

Kuhusu ubora wa barabara, Mhandisi Ndoveni alifafanua kuwa barabara hiyo inatengenezwa kwa uwezo wa kupitisha magari yenye uzito wa zaidi ya tani 30.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Huduma Saidizi TARURA, Azimina Mbilinyi ameeleza kuwa mradi huo umelenga katika kukuza uchumi wa wananchi na kuwezesha mizigo kuingia na kutoka viwandani kwa urahisi.

Bodi ya Ushauri ya TARURA inaendelea na ukaguzi wa miradi mbalimbali inayo tekelezwa katika Mikoa ya Morogoro, Pwani na Dar es Salaam.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles