26.2 C
Dar es Salaam
Monday, March 27, 2023

Contact us: [email protected]

Bodi ya Mikopo yapokea maombi 74,000, yaongeza siku tano

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imeongeza siku tano za wanafunzi kuendelea kuomba mkopo kwa njia ya mtandao hadi Agosti 23, lengo likiwa ni kutoa fursa kwa waombaji ambao hawajakamilisha maombi yao.

Taarifa ya HESLB kwa umma iliyotolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa bodi hiyo, Abdul-Razaq Badru, ilisema kuwa walianza kupokea maombi ya mikopo Julai Mosi, mwaka huu na mwisho ilikuwa iwe jana.

Alisema Badru katika taarifa yake kuwa HESLB imepokea maombi kutoka kwa baadhi ya waombaji mikopo ambao hawajakamilisha maombi yao kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kukosa nyaraka muhimu.

 “Ingawa hadi leo (jana) tumeshapokea maombi zaidi ya 74,821 yaliyokamilika kwa njia ya mtandao, tumepokea pia maombi kutoka kwa wateja wetu wakitaka kuongezewa muda ili wakamilishe nyaraka muhimu kama nakala za vyeti vya vifo vya wazazi wao, barua kutoka kwa wadhamini wao na nyaraka nyinginezo, tumewasikiliza na kuongeza muda,” alisema Badru.

 Aliwataka waombaji mikopo ambao hawajakamilisha maombi yao, kutumia muda ulioongezwa kukamilisha maombi yao kwa kuwa hawataongeza muda zaidi baada ya Agosti 23.

 “Tunasihi waombaji wetu watumie muda huu ulioongezwa kukamilisha maombi yao kwa kuwa hatutaongeza tena.

“Baada ya Agosti 23 tutaanza kufanya uchambuzi wa maombi tuliyopokea ili tuwapangie mikopo wenye sifa kwa wakati na tupeleke fedha za mikopo vyuoni kabla vyuo havijafunguliwa,” alisema Badru.

Katika kipindi kilichoongezwa cha hadi Agosti 23, Badru alisema dawati la huduma kwa wateja la HESLB litakuwa wazi ili kutoa ufafanuzi kwa waombaji mkopo pale utakapohitajika.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,206FollowersFollow
564,000SubscribersSubscribe

Latest Articles