24.1 C
Dar es Salaam
Tuesday, October 8, 2024

Contact us: [email protected]

Bodi ya makamishna ya kamisheni ya utalii Zanzibar yatembelea hifadhi ya taifa Ruaha

Na Mwandishi wetu Iringa.

Bodi ya Makamishna ya Kamisheni ya utalii Zanzibar ikiongozwa na Mwenyekiti wa Bodi hiyo Nd. Rahim Bhaloo imetembelea Hifadhi ya Taifa Ruaha Septemba 25,2024. Dhumuni la Safari hiyo ni kuangalia fursa mbalimbali zilizopo ndani ya Hifadhi ya Taifa Ruaha ili kufanya Hifadhi hiyo kuwa moja ya zao la utalii kwa watalii kutoka nchi mbalimbali wanaotokea Zanzibar.

“Lengo kubwa linaloambatana na Safari hii ni kuweza kuuza utalii wa Tanzania kwa Vivutio vya Fukwe na Hifadhi kwa pamoja”alisema Bhaloo.

Na hivyo kuendelea kukuza ushirikiano baina ya Zanzibar na Tanzania bara.

Kwa upande wake Mkuu wa Hifadhi, Hifadhi ya Taifa Ruaha,Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi,Godwell Ole Meing’aki alisema huduma za kitalii katika Hifadhi hiyo zimekuwa zikiimarika kila siku.

Aliipongeza bodi hiyo kwa kitendo cha kutembelea Hifadhi ya Taifa Ruaha ambapo alisema ushirikiano wao na wadau mbalimbali kunachangia shughuli za kitalii katika hifadhi hiyo kwa ujumla.

Aliongeza kuwa yapo maeneo mengi ya uwekezaji ndani ya Hifadhi na kuwa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania limeweka mazingira rahisi Kwa wawekezaji wa ndani na nje ya Taifa na kuwa milango ipo wazi Kwa yeyote atakae penda kuwekeza Hifadhi ya Taifa Ruaha.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles