28.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Bodi ya Ligi yabadili program Yanga

Na ZAINAB IDDY – DAR ES SALAAM

HATUA ya kupeleka mbele kwa mechi ya Watani wa jadi, kimebadili programu ya mazoezi ya timu ya Yanga.

Kikosi cha Yanga kiliingia kambini katika eneo la Kigamboni Jumanne ya wiki hii kwa ajili ya kujiandaa na mchezo dhidi ya Simba,uliokuwa umepangwa kuchezwa Oktoba 18 mwaka huu.

Hata hivyo,jana bodi hiyo iliusogeza mbele mchezo huo hadi Novemba 7 mwaka huu, ikitaja sababu ya kufanya hivyo kuwa ni kuwapo kwa uwezekano wa kukosekana kwa baadhi ya wachezaji wa timu hizo walioitwa timu za taifa kutokana na masharti ya usafiri yaliyowekwa na nchi mbalimbali kutokana na janga la corona.

Kutokana na mabadiliko hayo, benchi la ufundi la Yanga chini ya kocha,Juma Mwambusi limetoa fursa ya wachezaji wa timu hiyo kuendelea na mazoezi binafsi.

“Awali tulianza na programu ya kufanya mazoezi asubuhi na jioni, nilitenga muda wa siku tano kwa wiki kasoro Jumamosi na Jumapili, kabla ya kuja kufanya tasmini ambayo ingetupa muongozo wa nini cha kufanya katika wiki ya mwisho kuelekea mchezo wetu na Simba.

“Lengo la kufanya hivi lilikuwa  kuwajenga fiziki na utimamu wa miili  wachezaji wetu lakini baada ya taarifa ya mabadiliko ya mechi hiyo na urefu wa muda uliopo kabla ya kuja kucheza na Biashara United, nimetoa ruhusa kwa wachezaji kutumia muda mwingi kufanya mazoezi binafsi, nikiwa na maana yale ya timu yatakuwa yanafanyika kwa kipindi kimoja,” alisema Mwambusi.

Akizungumzia hali za wachezaji wake kwa ujumla, Mwambusi alisema wapo katika hali nzuri kuelekea kipindi hiki kirefu cha mapumziko, lakini watahakikisha viwango vya wachezaji vinabaki katika hali nzuri muda wote.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles