23.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

BODI VETA YATAKIWA KUTEKELEZA MIRADI YA MAENDELEO MAPEMA

Na: Frank Shija, MAELEZO


BODI ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) imeagizwa kuanza mara moja kutekeleza miradi ya maendeleo.

Miradi hiyo ni ambayo utekelezaji wake umekuwa ukisuasua kwa muda mrefu huku kukiwa na fedha zilizotengwa kwa ajili ya utekelezaji miradi hiyo.

Agizo hilo limetolewa na Waziri wa Elimu, Sayansi na Mafunzo Stadi, Profesa Joyce Ndalichako, wakati akizindua bodi mpya ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ya Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi   Dar es Salaam jana.

Profesa Ndalichako alisema ameshangazwa na kitendo hicho cha ucheleweshaji wa utekelezaji wa miradi hiyo huku kukiwa na  takriban Sh bilioni 14.5 zilizotengwa katika bajeti ya mwaka wa fedha 2016/207 kwa ajili ya kazi hizo.

“Inasikitisha kuona kuwa tunakaribia robo ya mwisho ywa mwaka wa fedha 2016/2017 huku karibu miradi yote ya maendeleo haijaanza kutekelezwa isipokuwa ile tu ya kujengea uwezo na siyo ya ujenzi wa VETA ambazo ndiyo mahitaji makubwa kwa sasa,” alisema .

Alisema bodi hiyo inapaswa kuanza kazi mara moja ikiwa ni pamoja na kuwachukulia hatua watendaji watakaobainiuka kuhusika katika kuchelewesha kuanza   miradi hiyo.

  Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Peter Maduki amempongeza waziri N kwa kuwa muwazi katika kuelezea kutoridhishwa na udhaifu katika utendaji kwa baadhi ya wafanyakazi wa mamlaka hiyo.

Aliahidi kushughulikia suala hilo huku akiwataka wajisahihishe badala ya kusubiri kuwajibishwa.

 Awali,   Kaimu Mkuu wa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) Dk. Bwire Ndazi alisema changamoto kadhaa katika eneo hilo   kuwa ni pamoja na uwezo mdogo wa VETA na wadau katika kufikia mahitaji ya elimu na mafunzo ya ufundi.

 Alitoa mfano kuwa watu wanaohitaji kujiunga na mafunzo wanakadiriwa kuwa 600,000 kwa mwaka wakati uwezo wa vyuo vyote vya VETA, vya Serikali na binafsi ni   125,000 tu kwa mwaka.

Bodi iliyomaliza muda wake iliundwa Agosti 2011 na kumaliza muda wake kisheria Agosti 2014, na baadaye kuongezewa muda hadi Desemba  2016.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles