24.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 16, 2024

Contact us: [email protected]

Bodaboda waonywa vurugu wakati wa Uchaguzi Mkuu

Na Ahmed Makongo, Bunda

WAENDESHA pikipiki maarufu kwa jina la bodaboda wilayani Bunda mkoani Mara, wametakiwa kutokurubuniwa na kuingia kwenye vurugu wakati huu wa kuelekea Uchaguzi Mkuu.

Wametakiwa pia kuwa makini na baadhi ya wagombea wa nafasi mbalimbali ambao wanaweza kuwashawishi kwa kuwapa mafuta ili kusababisha uvunjifu wa amani.

Wito huo umetolewa jana na Mkuu wa Wilaya hiyo, Lydia Bupilipili, wakati wa mafunzo ya kuwajengea uelewa bodaboda hao juu ya huduma ya kwanza baada ya ajali.

Mafunzo hayo yaliyoendeshwa na Chama cha Msalaba Mwekunduku (Red cross) mkoani Mara.

Bupilipili alisema wapo baadhi ya wagombea hawana nia njema na raia pamoja na nchi kwa ujumla, hivyo bodaboda wasitumike vibaya katika kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu.

Aliwataka kuwa makini maana wanaweza kuishia pabaya, ikiwemo kupata ulemavu wa kudumu kwa maslahi ya watu wengine ambayo hayana tija kwa taifa.

“Bodaboda msiingie kwenye vurugu kipindi hiki cha uchaguzi na muwe makini na wagombea msije mkapewa lita za mafuta mkasahau sheria za nchi, wapo wagombea wengine hawana nia njema na raia,” alisema Bupilipili.

Katika hatua nyingine aliwataka bodaboda kuwa na bima ikiwemo ya afya, ili wanapopata changamoto ya kuugua au ajali bima iweze kuwasaidia.

Aliwataka pia kuboreshahuduma zao kwa kuwa wasafi  na kutoa lugha nzuri kwa wateje wao.

Aidha, alisema Serikali inatambua mchango mkubwa wa bodaboda hao kwa sababu wanawasaidia sana katika suala zima la ulinzi na usalama, ambapo mambo mengi wanayapata kupitia kwao.

“Tunatambua mchango wa bodaboda maana wanatusaidia sana kwenye mambo ya ulinzi na usalama kwani kuna mambo mengi tunayapata kupitia bodaboda kutokana na shughuli zenu” alisema.

Awali Mwenyekiti wa Red cross Mkoa wa Mara, Frank Bwire, alisema lengo la mafunzo hayo ni kuwa na huduma kwa ukaribu zaidi hasa kwa kundi hilo la bodaboda kwani wao ni wahanga wakubwa, ambapo hawana uelewa juu ya huduma ya kwanza baada ya ajali kutokea.

“Kwa kuwa tuko kwenye uchumi wa kati basi tukabiliane na kwenda sawa na hali ya sasa, kwani hata uchumi ukuwa kwa kuwa na usalama na huduma ya kwanza,” alisema.

Bwire alisema zoezi hilo ni endelevu kwa wilaya zote za mkoa wa Mara.

Mmoja wa wawezeshaji katika mafunzo hayo Athanas Lubuka, alisema kuwa bodaboda wengi hupata ajali kwa sababu ya uzembe wao, ambapo pia aliwataka kuwa na masanduku ya huduma ya kwanza kwenye pikipiki zao, ili kuepukua kupoteza maisha ama kupata ulemavu wa kudumu, pindi wapatapo ajali.

Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani katika Wilaya ya Bunda Rose Mbaga, aliwataka bodaboda kuzingatia sheria za usalama barabarani na usafirishaji hasa kipindi hiki cha kuelekea katika uchaguzi mkuu.

“Sisi tunayo mamlaka ya kukamata na kuzuia chombo endapo dereva hafuati sheria za usalama barabarani na usafirishaji.

 “Na msiwe mbelembele kuendesha pikipiki ovyo acheni wao watangulie kwani huenda wakawaacha katika taabu baada ya uchaguzi,” alisema Mbaga.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles