28.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, June 6, 2023

Contact us: [email protected]

Bodaboda wahimizwa kupinga vitendo vya ukatili

Na Beatrice Kaiza, Mtanzania Digital

MADEREVA wa Bodaboda wametakiwa kuwa mstari wa mbele katika kupinga na kukomesha vitendo vya ukatili kwa wanawake na watoto ili kunusuru taifa la kesho.

Kauli hiyo imetolwa leo Machi 20, 2023 na Mkuu wa Chuo cha Ustawi wa Jami, Joyce Nyoni wakati wa kufungua mafunzo kwa Viongozi wa madereva bodaboda katika Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Nyoni amesema kuwa wanahitaji kuhakikisha vitendo vya ukatili vinaisha kwani mtoto anaweza kafanyiwa ukatili akiwa mdogo ambapo yanaharibu mahusiana yake na maisha wakati wa ukubwani.

Ukatili unamadhara ya kisaikolojia ambapo inaonekana kidonda kinapona lakini yale madhara yakisaikolojia huwa hayaponi na hasa kama hajapata huduma stahiki kwa wakati.

“Tunaomba kama sehemu ya jamii kutokana na kazi zenu mnakutana na watu wengi mnabeba wadada,watoto ingawa wanasema watoto ni taifa la kesho sisi tunasema ni taifa la leo kwamba jinsi utakavyomlea leo ndio unavyotengeneza kizazi kijacho,” amesema Nyoni.

Aliongeza kuwa Leo wewe ni kijana unaguvu kesho unakuwa mtu mzima je hiki kizazi kinachofata huku nyuma unataka kiweje sisi tunaona mnamchango mkubwa kuhakikisha jamii inastawi sawa sawa.

Kwa upande wa Mratibu wa kitengo cha ushiriki jamii na wa mafunzo , Dastan Haule amesema walilenga kukutana na makundi la viongozi wa waendesha bodaboda kwa kuwajenge uwezo ili wao waweze kuongea na wenzao .

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,307FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles