25.2 C
Dar es Salaam
Monday, December 2, 2024

Contact us: [email protected]

BODABODA WAHASWA KUVAA ‘REFLECTOR’ KUEPUSHA AJALI

Brighiter Masaki – Kisarawe.

Mkuu wa Usalama Barabarani, Wilaya ya Kisarawe, Novatus Mallya, amewataka madereva wa boda boda kutii, kufata taratibu na sheria za Barabarani kwa kuvaa kofia, viatu na vizibao vya kuakisi mwanga (reflector) ili kupunguza ajali za mara kwa mara.

Akizungumza na Mtanzania mapema leo Oktoba 14 wakati alipokuwa akipokea zawadi ya vizibao vya madereva wa bodaboda kutoka kwa Bishara Njema Foundation anasema kuwa ni wakati wa bodaboda kujituma na kujitambua kama wafanyakazi wengine. 

“Nawashukuru Bishara Njema Foundation kwa kushirikiana na diwani kwa kuokoa maisha ya vijana wanaojitafutia riziki. Niwaombe madereva mzidi kufuata sheria za usalama barabarani, zitawasaidia kufikia malengo na kutokatisha maisha kwa haraka, reflector inasaidia hata usiku mtu kukuona na kujua kuna bodaboda anakuja,” anasema Mallya. 

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bishara Foundation, Nunu Rashidi, anasema wameamua kutoa vizibao ili kuwasaidia madereva wajiepushe na ajali wanapokuwa kwenye vyombo vya moto, akieleza kuwa ushirikiano huo utaendelea zaidi.  

Aidha Diwani wa Kisarawe, Abel Mudo, anasema anawapongeza bodaboda kwa nidhamu kubwa waliyonayo katika kupigania usalama wa wananchi na kuwaomba waendelee hivyo hivyo. 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles