24.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 24, 2023

Contact us: [email protected]

Bodaboda huua 800, kila mwaka 3,700 hupoteza viungo

Mwandishi wetu, DodomaZaidi ya watu 800 hufariki dunia kila mwaka kutokana na ajali za barabarani huku zaidi ya 3,700 wakipoteza viungo vyao.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamadi Masauni, ameyasema hayo leo wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu, Fakharia Khamis.

Akijibu swali hilo, Masauni amesema tangu mwaka 2008 wakati ambao usafiri wa pikipiki maarufu bodaboda na bajaji zilianza kutumika kama vyombo vya usafiri rasmi hadi kufikia Septemba mwaka huu, vyombo hivyo vimesababisha ajali 38,237.

“Watu waliopoteza maisha kutokana na ajali za bodaboda tangu mwaka 2008 hadi Septemba mwaka huu ni 8,237 (sawa na watu 823 kila mwaka), waliopoteza viungo katika kipindi hicho ni 37,521 (sawa na watu 3,752 kila mwaka),” amesema Masauni.

Amesema Serikali haitakubali kuona watu wengi hivyo wakipoteza maisha hivyo, wataendelea kusimamia kanuni na sheria kudhibiti hali hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,074FollowersFollow
563,000SubscribersSubscribe

Latest Articles